Balozi wa Denmark nchini Mhe. Mette Dissing-Spandet akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa leo tarehe 26 Julai 2020 jijini Dar es Salaam 
Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
Baadhi ya mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na mama Anna Mkapa mara baada ya kutoa salamu za pole nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi wa Ubalozi wa Uganda nchini Bibi. Musekura Eseza akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Sweden nchini Bw. Michael Sulusi akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa  
Mwakilishi wa Ubalozi wa Sudan nchini Bw. Jaafar Nasir Abdalla akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa 
Mwakilishi wa Ubalozi wa Uturuki nchini Bw. Onur Yay akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa Balozi wa Hispania nchini Mhe. Fransisca Pedros akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa leo tarehe 26 Julai 2020 jijini Dar es Salaam
Balozi wa Morocco nchini Mhe. Abdelilah Benryane akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa 
Balozi wa Zambia nchini Mhe. Benson Keith Chali akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
Balozi wa Congo DRC nchini Mhe. Jean -Pierre Mutamba akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
Balozi wa Somalia nchini Mhe. Mohamed Hassan akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa

Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, wameendelea kujitokeza kusaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa na kumuelezea kuwa ni kiongozi mahiri na msuluhishi nguli wa amani barani Afrika na duniani.

Mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, baadhi ya mabalozi hao wakaelezea walivyoguswa na msiba wa Mkapa na kusema Tanzania imepoteza kiongozi na msuluhishi nguli wa amani barani Afrika na duniani.

Kwa upande wake, Balozi wa Zambia nchini Mhe. Benson Keith Chali amesema kuwa Zambia wameguswa sana na msiba kwani Tanzania na Zambia ni ndugu, “toka mwanzoni Nyerere na Kaunda walikuwa ndugu na sisi tumeendelea kuwa ndugu na unapopoteza ndugu unaumia sana. Sisi kama Zambia kwa kweli tumepokea kwa masikitiko makubwa tarifa za kifo cha Mzee Mkapa,” .

“Tutamkumbuka Mzee Mkapa kama kiongozi aliyesimamia amani maeneo mbalimbali barani Afrika ikiwemo Kenya, Burundi, Congo DRC, na kwingineko duniani,” amesema Mhe. Keith Chali 

Mhe. Keith Chali ameendelea kusema kuwa “Sisi kama Zambia tunatoa sana pole kwa familia yake, Serikali ya Tanzania na Watanzania kwa ujumla ……tunaomboleza wote msiba huu mzito,”.

Nae Balozi wa Denmark nchini Mhe. Mette Dissing-Spandet amesema kuwa Rais Mstaafu Mzee Mkapa alikuwa kiongozi mahiri kwa Tanzania lakini pia alikuwa rafiki na mfano wa kuigwa na mataifa mbalimbali.

“kwetu sisi kama Denmark alikuwa rafiki na tutaendelea kumkumbuka daima kwa upendo wake,” Amesema Mhe. Mette.

Aidha, nae Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal amesema kuwa Mzee Mkapa alikuwa mtetezi wa amani barani Afrika na atakumbukwa kwa mema aliyoyafanya kwani aliyafanya kwa jitihada na weledi wa hali ya juu, Mungu ampumzise kwa Amani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: