Makatibu Wakuu kutoka Sekta za Mazingira, Maliasili na Uvuvi kutoka kushoto; Mhandisi Joseph Malongo, Dkt. Aloyce Nzuki, Prof. Adolf Mkenda na Dkt. Rashid Tamatamah wakikagua maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii hii leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC). Makatibu Wakuu hao wameridhishwa na maandalizi ya Mkutano huo ambayo yamekamilika kwa asilimia 100.
Picha ya Pamoja ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri Mazingira,Maliasiki na Utalii wa nchi wananchama wa SADC unaotarajiwa kuanza kesho Jijini Arusha.
Na Vero Ignatus, Arusha.
Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii wa nchi mwanachama wa SADC unaotajia kuanza kesho jijini Arusha yamekamilika na tayari kutoka mataifa mbalimbali wameanza kuwasili jijini Arusha kwa ajili ya kuanza mkutano huo kesho.
Peofesa Adolf Mkenda ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliadili na Utalii amesema maandalizi tayari yamekamilika kuanzia eneo ambalo mkutano huo utafanyikia usafiri,chakula pamoja na fursa ya kutembelea hifadhi mbalimbali za taifa itakayokuwepo katika kipindi chote cha mkutano.
Profesa Mkenda amesema kuwa siku ya kesho makatibu wakuu wa Wizara husika watakutana na kuandaa agenda za mkutano huo ambao mpaka sasa maandalizi yamekamilika.
Dr,Omar Ali Amir ni Naibu Katibu Mkuu ,Wizara ya Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar ameeleza kuridhishwa na maandalizi yaliyofanyika mpaka sasa na Tanzania na chi za SADC zitaweka mikakati ya kushirikiana katika kupambana na uvuvi haramu baharini na kusimamia sambamba rasilimali za uvuvi.
Mhandisi Joseph Malongo ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Raisi ,Muungano na Mazingira ,amesema katika mkutano huo kuna mambo makubwa ambayo watahimiza ikiwemo nchi ambazo haziridhia kuanzishwa kwa itifaki ya SADC ziweze kuridhia ikiwa ni pamoja na kupitia na kutathmini mpango mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi wan chi za SADC.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Rashid Tamatama amesema kuwa miongoni mwa mambo muhimu watakayoyaangazia ni pamoja na itifaki ya Sadc inayolenga kuinua maisha ya watu kupitia sekta ya uvuvi ambayo eneo la kimkakati linalochangia katika usalama wa chakula na kukuza uchumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: