Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures Lucy Dominic akizungumza wakati wa sherehe ya pongezi na maombi ya shukrani kwa shule ya Msingi Little Treasures kushika nafasi ya nne kitaifa,nafasi ya kwanza wilaya ya Shinyanga na ya kwanza mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya kidato cha saba mwaka 2019.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Mohammed Kahundi akizungumza wakati wa sherehe ya pongezi na maombi ya shukrani kwa shule ya Msingi Little Treasures kushika nafasi ya nne kitaifa,nafasi ya kwanza wilaya ya Shinyanga na ya kwanza mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya kidato cha saba mwaka 2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Sehemu ya wanafunzi 91 waliomaliza darasa la saba katika shule hiyo na wote wamepata daraja A katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2019 na kuifanya shule hiyo kung'aa ngazi ya taifa,wilaya na mkoa wa Shinyanga.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akicheza na wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 2019 na kufaulu katika shule ya msingi Little Treasures leo. Jumla ya wanafunzi 91 wamemaliza darasa la saba katika shule hiyo na wote wamepata daraja A katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2019 na kuifanya shule hiyo kung'aa ngazi ya taifa,wilaya na mkoa wa Shinyanga.
Sehemu ya wanafunzi waliomaliza darasa la saba katika shule ya msingi Little Treasures wakiwa katika sherehe ya pongezi na maombi ya shukrani kwa shule ya Msingi Little Treasures kushika nafasi ya nne kitaifa,nafasi ya kwanza wilaya ya Shinyanga na ya kwanza mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya kidato cha saba mwaka 2019.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya msingi Little Treasures,Tilulindwa Sulusi akimuonesha mwanafunzi aliyeshika nafasi ya saba kitaifa katika matokeo ya darasa la saba 2019,Daniel Ngassa kutoka shule ya Little Treasures iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga. Wanafunzi wa kike waliosimama pia wamekuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa katika matokeo ya darasa la saba 2019.Kushoto ni Suzane Assenga na Scolastica Shelembi (kulia).
Meza kuu wakifuatilia matukio yanayoendelea.
Wazazi wa Daniel Ngassa wakimpongeza kijana wao kwa kushika nafasi ya saba kitaifa katika matokeo ya darasa la saba 2019.
Nabii Janeth Aminiel Kimo wa Kanisa la Uwezo wa Bwana Mwanza akiwaombea wanafunzi waliomaliza darasa la saba 2019 katika shule ya msingi Little Treasures na kufaulu vizuri katika mtihani.
Maombi yakiendelea kumshukuru Mungu kutokana na matokeo mazuri iliyopata shule ya msingi Little Treasures katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2019.
Askofu Raphael Machimu kutoka kanisa la EAGT Shinyanga akiendesha maombi ya shukrani kwa shule ya Msingi Little Treasures kushika nafasi ya nne kitaifa,nafasi ya kwanza wilaya ya Shinyanga na ya kwanza mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya kidato cha saba mwaka 2019.
Maombi yakiendelea kumshukuru Mungu kutokana na matokeo mazuri iliyopata shule ya msingi Little Treasures katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2019.
Padre Tupendane Philemon wa Kanisa Katoliki la Mt. Yosefu Mipa (Jimbo Katoliki la Shinyanga) akiwaombea wahitimu wa shule ya msingi Little Treasures na shule hiyo kwa ujumla.
Maalim/Ustadhi Ashiraf Majaliwa akitoa salamu za Mufti wa Tanzania na Sheikh wa mkoa wa Shinyanga na kuomba dua kwa ajili ya shule ya Little Treasures.
MC Mama Sabuni akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga (RTO) Anthony Gwandu (kushoto).
Wageni waalikwa wakiwa eneo la tukio.
Watahiniwa bora kitaifa matokeo ya mtihani darasa la saba 2019 kutoka shule ya Msingi Little Treasures (Daniel Ngassa katikati aliyeshika nafasi ya saba kitaifa) na Wanafunzi wa kike ambao ni miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa katika matokeo ya darasa la saba 2019 Suzane Assenga (kulia) na Scolastica Shelembi (kushoto) wakikata keki.
wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Wahitimu darasa la saba 2019 shule ya Little Treasures wakicheza wimbo wa Yope wa Diamond na Innoss'B
Wahitimu darasa la saba 2019 shule ya Little Treasures wakicheza wimbo wa Yope wa Diamond na Innoss'B
Mwalimu Mkuu shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akizungumza wakati wa sherehe na maombi kwa shule ya Little Treasures
Walimu wa shule ya msingi Little Treasures wakitoa burudani ya wimbo.
Meneja wa Shule ya msingi Little Treasures Wilfred Mwita akizungumza wakati wa sherehe ya pongezi na maombi ya shukrani kwa shule ya Msingi Little Treasures kushika nafasi ya nne kitaifa,nafasi ya kwanza wilaya ya Shinyanga na ya kwanza mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya kidato cha saba mwaka 2019.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Shinyanga Neema Mkanga akizungumza wakati wa sherehe ya pongezi na maombi ya shukrani kwa shule ya Msingi Little Treasures kushika nafasi ya nne kitaifa,nafasi ya kwanza wilaya ya Shinyanga na ya kwanza mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya kidato cha saba mwaka 2019.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya msingi Little Treasures,Tilulindwa Sulusi akikabidhi keki maalumu kwa wahitimu wa darasa la saba mwaka 2019
Zoezi la kukabidhi keki likiendelea.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga imefanya sherehe ya kujipongeza na maombi ya shukrani kwa kupata matokeo mazuri katika mtihani wa taifa wa darasa la saba mwaka 2019 wakiongoza na kauli mbiu 'Tanzania Four, Shinyanga One'.
Shule ya Little Treasures imeshika nafasi ya nne katika orodha ya shule 10 bora kitaifa huku mwanafunzi Daniel Ngassa kutoka shule hiyo akishika nafasi ya saba kwenye orodha ya watahiniwa bora kitaifa na wanafunzi wengine wawili ambao ni Suzane Assenga na Scolastica Shelembi wakiingia kwenye orodha ya watahiniwa bora 10 kitaifa upande wa wasichana.
Sherehe ya Pongezi na Maombi kwa shule hiyo imefanyika leo Jumamosi Oktoba 19,2019 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi,viongozi wa dini madhehebu mbalimbali,wageni waalikwa,wazazi na walezi,walimu na wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 2019.
Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Little Treasures Lucy Dominic amesema shule hiyo imeshika nafasi ya nne kitaifa,ya kwanza katika wilaya ya Shinyanga na ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga hivyo lengo la sherehe na maombi hayo ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda na kuiinua shule hiyo.
"Tuko hapa kwa lengo kuu la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda na kuiinua shule yetu. Tunaamini kuwa ni Mungu pekee anaye tuwezesha, Ni nafasi pia kuendelea kuomba neema zake azidi kutubariki zaidi na zaidi kwani Sisi kama wanadamu tunajua tulikotoka na tulipo lakini hatujui tunakokwenda na ndiyo maana tunamtanguliza mbele azidi kuwa nuru yetu",alisema Dominic.
"Tumekutana hapa ikiwa ni mwendelezo wa furaha isiyo kifani kwetu wanafamilia ya Little Treasures. Kumshukuru Mungu na kusherehekea mafanikio makubwa tuliyoyapata katika matokeo ya mtihani wa tiafa wa darasa la saba mwaka 2019",aliongeza.
Kwa upande wake,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi aliipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 na kuahidi kutoa zawadi kwa shule na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mtihani.
"Little Treasures mmefanya maajabu,tunawapongeza sana,mmeutangaza mkoa wetu,mmeuingiza mkoa wetu katika shule 10 bora kitaifa",alisema Kahundi.
"Nazipongeza Shule zetu tatu binafsi ambazo ni Little Treasures,Kwema Modern na Rocken Hill kwa kweli zimetangaza mkoa wetu kwa matokeo mazuri kitaifa.Lakini nizipongeze shule za serikali za mkoa wa Shinyanga ambazo zimefanya vizuri kwenye matokeo haya nazo ni Kinaga iliyopo Kahama,Ilobi iliyopo Kishapu na Mwenge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga",alisema Kahundi.
Alisema mbali na mkoa wa Shinyanga kushuka kutoka nafasi ya 15 mwaka 2018 hadi 17 mwaka huu akitaja sababu kuu kuwa ni wanafunzi kuacha shule ' Drop outs',shule za serikali zimeendelea kufanya vizuri kwenye mitihani.
Toa Maoni Yako:
0 comments: