Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Selemani Jafo akizungumza alipotembelea katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.

Na Mwandishi Wetu.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa Tamasha la utamaduni na sanaa la nchini za Afrika mashariki litumike kukiuza kiswahili ili na nchini mwanachama wa Afrika Mashariki waweze waongee lugha hii adhimu ambayo sasa ni lugha rasmi katika jumuiya za Afrika.

Amesema hayo alipotembelea maonesho ya Tamasha la Uatamaduni na Sanaa la nchi za Afrika amashariki al-maalufu kama JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwa nja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

"Nimetembelea mabanda mbalimbali na kujionea bidhaa mbalimbali za asili na utamaduni wa maeneo mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki za wajasiriamali wa nchi zote".

Amesema kuwa wizara ya Tamisemi ni chumvi, Afya, elimu vipo chini ya wizara yake, lakini wizara ya habari utamaduni, Sanaa na Michezo hususani Maafisa Utamaduni wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri wako TAMISEMI, hivyo unaweza kuona kwanini yupo hapa.

Hata amewapongeza wizara ya habari na utamaduni kwa kufanya kazi nzuri pamoja na kuhakikisha tamasha hili linafanyika kama lilivyopangwa na kwa mafanikio makubwa hasa kukidhi kiu ya wananchi wanaohudhuria tamasha hili adhimu.

"Sina cha kuficha, nimefurahishwa na mambo yote niliyoyaona hapa uwanja wa Taifa hakina mmejipanga vyema, hongerani sana," amesema.

Pia amesema kuwa amefurahishwa na maandalizi ya Tamasha la JAMAFEST na amewasihi wananchi kuja kwenda Uwanja wa Taifa kujifunza tamaduni mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (mwenye tai nyekundi) akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Yusuph Singo (wa kwanza kushoto) wakati alipotembelea katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. 
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Selemani Jafo akimsikiliza mkuu wa kikundi cha kukuna nazi ikiwa washiriki ni washindi katika makundi mbalimbali walioshindanishwa kukuna nazi. Mashindano hayo yanafanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Tanzania katika maonesho ya Tamasha la JAMAFEST. Ikiwa wamepata washindi wa tatu kutoka makundi tofauti wakiwa wananwake wawili pamoja na mwananume mmoja.
Akina mama wakikuna nazi katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri Jafo akiangalia nazi iliyokunwa vizuri katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri Jafo akitoa neno katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri Jafo akijionea sanaa za mikono katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mchezo wa mdako ukiendelea katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mchezo wa bao ukiendelea katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Selemani Jafo akiangalia meza na viti vilivyotengenezwa na Mianzi. Yote hayo ni katika tamasha la JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwanja wa Taiafa jijini Dar es Salaam.
Waziri Jafo akijionea shughuli za mikono zinazofanywa na wajasiliamali toka katika jumuiya ya Afrika Mashariki katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: