Wachezaji ngoma wa Kinyarwanda wamesimamisha kwa muda shughuli nyingine zilizokuwa zikiendelea kwenye maonyesho ya Tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki (JAMAFEST) jijini Dar es Salaam nchini Tanzania baada ya kupanda jukwaani.
Watazamaji mbalimbali kwenye maonyesho wameacha shughuli zao kwa muda na kusogea kushuhudia ngoma hiyo iliyoshirikisha wanaume na wanawake.
Wadada wa Kinyarwanda walikuwa kivutio zaidi huku baadhi ya watazamaji wakiwashangilia na wengine wakionyesha kuwakubali kwa kuchukua video kwa simu na wengine wakijadiliana kuhusu urembo wa wanawake wa Kinyarwanda.
“Huwa nashangaa hawa kina dada kutoka nchini Rwanda ni warembo jamani “Halafu hawatumii mavitu vitu lakini kama wananyumbulika.”
“Nikiwaona kwenye picha huwa nahisi wamejiumba wenyewe jinsi wanavyovutia kama wamezaliwa na mama mmoja..” walisikia vijana wawili waliokuwa wakizungumza uwanja hapo wakati ngoma hiyo ikiendelea kutumbuiza
Walisikika baadhi ya watu uwanjani hapo kila mmoja akisema lake kuhusu urembo wa wanawake hao ambao umekuwa gumzo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: