08/01/2019 - 09/01/2019
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kulia),Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (wanne kulia), Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Fortunatus Musilimu(watano kulia) na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Kamishna Msaidizi Jumanne Muliro(wapili kulia) wakiwaongoza mabalozi wa usalama barabarani na wananchi wakati wa maandamano ya amani lengo ikiwa kuhamasisha masuala ya usalama barabarrani ili kuepusha ajali za barabarani,maandamano hayo yamefanyika leo jijini Mwanza.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akipaka rangi za pundamilia katika sehemu ya kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo la mabatini wakati wa kuadhimisha Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani leo jijini Mwanza.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msadizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu akipaka rangi za pundamilia katika sehemu ya kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo la mabatini wakati wa kuadhimisha Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani leo jijini Mwanza.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro akipaka rangi za pundamilia katika sehemu ya kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo la mabatini wakati wa kuadhimisha Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani leo jijini Mwanza.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mwenywekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza,Ferdinand Chacha, akimwaga chenga maalumu ambazo huonyesha sehemu ya kivuko nyakati za usiku, katika sehemu ya kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo la mabatini jijini Mwanza wakati wa kuadhimisha Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani leo jijini Mwanza.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mabalozi wa Usalama Barabarani wakiwa katika maandamano ya amani yenye lengo la kuhamasisha Usalama wa Barabarani wakati wakuhadhimisha siku ya mabalozi hao iliyofanyika leo jijini Mwanza.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Wadau wa mazao ya nafaka, wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe. Japhate Hasunga wakati akihutubia mkutano wa siku mbili wa Wafanyabiashara wa Nafaka Ndani na Nje ya Nchi kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam 
Mhe. Waziri Hasunga.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akihutubia mkutano huo.
Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt.Hoseana Lunogelo, akiwasilisha mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).
Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt.Hoseana Lunogelo, akiwasilisha mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).
Bi. Margareth Nzuki (katikati), akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF akifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inawasilishwa na Dkt. Bunogelo kuhusu utafiti ambao ulifanywa na Taasisi hiyo kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).
Mkuurgenzi Mtednaji wa Benki ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw.Japhet Justine akipiga makofi wakati mkutano huo ukiendelea.
Mjumbe akifuatilia kwa makini mkutano huo.
Mjumbe akifuatilia kwa makini mkutano huo.
Bi.Margareth Nzuki (kushoto), kutoka ESRF akibadilishana mawazo na Bi. Vumilia L. Zikankuba kutoka Wizara ya Kilimo wakati wa mkutano huo.
Mshiriki akitoa maoni yake.
Oswald Mashindani (kushoto), kutoka ESRF akizunhumza jambo mbele ya Katibu Mkuu (mstaafu) Wizxara ya Fedha, Bw. Paniel Lyimo (katikati) wakati wa mkutano huo.
Mhe. Hadsunga (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na manaibu waziri makatibu wakuu na Mwenyekiti wa TPSF.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID.

MKUTANO wa siku mbili wa Wafanyabiashara wa Nafaka Ndani na Nje ya Nchi umefunguliwa na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Agosti 29, 2019.

Mkutano huo ambao umewajumuisha wasindikaji, wasafirishaji na wamiliki wa maghala ya nafaka Lengo lake ni kuangalia fursa zilizopo kwenye tasnia ya nafaka na jinsi ya kuzifikia ikiwa ni pamoja na masoko.

Akizungumza na washiriki wa mkutano huo uliowakutanisha wadau kutoka mikoa mbalimbali nchini, Mhe. Hasunga ambaye alifuatana na Manaibu wake, Mhe. Husein Bashe, na Mhe. Omary Mgumba alisema mkutano huo utatoa fursa kwa wajumbe kuelimishwa kuhusu fursa ya biashara ya mazao ya nafaka katika soko la Afrika, uwezo wa Tanzania kuzalisha na nafasi ya wafanyabiashara kushiriki kikamilifu lakini pia washiriki watapata fursa ya kujifunza athari za upotevu wa mazao ya nafaka baada yamavuno na mkakati wa serikali kudhibidi hali hiyo.

“Kitaalamu wanasema utafiti uliofanyika Tanzania na nchi nyingi za Kusini asilimia 40 ya mazao yote yakiwemo ya nafaka yanapotea baada ya mavuno kwa kuharibika na matatizo mengine, hii haikubaliki mkulima amewekeza, amevuna halavu mazao yake yanaharibika, lazima tuwe na mkakati wa kuzuia hali hii.” Alitoa hakikisho Mhe. Waziri Hasunga na kuongeza.

Kulingana na uzalishaji uliopo, nafaka nyingi kama mahindi mtama na nafaka nyingine huhifadhiwa katika kiwango kisichoridhisha hali hii huchangia kupoteza ubora wa nafaka na hatimaye huchangia kuzorota kwa ustawi wa afya zetu, alifafanua zaidi Mheshimiwa Waziri.

Alisema Agosti 1, mwaka huu kwenye sherehe za Nanenane kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganow a Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alizindua mkakati wa namna ya kupambana na kudhibiti upotevu wa mazao baada ya mavuno.

Katika utafiti wake ilioufanya hivi karibuni Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya Mradi wa Rapid Response Implementation Support to the Ministry of Agriculture and Agriculture Sector Lead Ministry (RARIS) unaofadhiliwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation umebaini kuwa hali ya maghala mengi ya watu binafsi hayatoi taarifa serikalini na hii ni kutokana na mfumo wa sasa wa maghala.

Akitoa mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses), Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt.Hoseana Lunogelo alisema ESRF ilifanya utafiti wa hali (status) ya maghala nchini na kubaini kuwa maghala ya watu binafsi hayalazimiki kisheria kutoa taarifa serikalini kuhusu nini kimehifadhiwa na kiasi gani cha nafaka kilichohifadhiwa ndani ya maghala hayo na hali hii serikali inategemea tu maghala ya Serikali yaani (Public Storage Facilities ) kupitia Werehouse Reseat Regulatory Board ili kujua takwimu za hali ya chakula nchini.

“Kwa sasa kuna maghala 3,430 yaliyopo kati ya hayo ni 185 tu ndiyo kuna uhakika wa kupata tawimu endapo zitahitajika lakini yaliyosalia huwezi kupata takwimu hizo kwa sababu hakuna sheria inayowalazimisha kufanya hivyo.” Alifafanua Dkt. Lunogelo.

Alisema hii ni changamoto kubwa, kama serikali inapata taarifa kutoka kwenye maghala machache sana nchini na yale mengi haipati taarifa zake, maana yake Serikali haiwezi kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na upatikanaji wa chakula nchini na hiyo ina athari mbaya kwenye usalama wa chakula na pia ina athari mbaya pia kwenye biashara.” Alsiema Dkt. Lunogelo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio akipeana mkono na Mtendaji Mkuu wa Chiyoda Corporation Ndg. Ken Nagao baada ya kikao baina ya ujumbe wa Tanzania na Kampuni ya Chiyoda. Wengine pichani kutoka kushoto ni Ndg. Pius Gasper (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Innocent Luoga, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu (Wizara ya Nishati), Ndg. Katsuo Nagasaka (Chiyoda) na Ndg. Koji Nishita (Chiyoda).
Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika kikao na Kampuni ya JGC kilichofanyika sambamba na kilele cha Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD7). Upande wa kushoto ni Ndg. Kenji Yamamoto (JGC), Ndg. Masayuki Sato (JGC), Ndg. Yanamaka (JGC) na Ndg. Taketoshi Shogenji (JGC). Upande wa Kulia ni Mhandisi Innocent Luoga, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu (Wizara ya Nishati), Dkt. James Mataragio, Mkurugenzi Mtendaji (TPDC) na Ndg. Pius Gasper (Tanesco).

Na Mwandishi Wetu - Yokohama, Japan.

Kampuni kubwa za Japan zenye uzoefu wa miaka mingi katika miradi ya gesi asilia zimeonesha nia ya kuwekeza nchini Tanzania hususan katika mradi mkubwa wa kusindika gesi asilia (Liquefied Natural Gas-LNG). Kampuni za JGC na Chiyoda zenye uzoefu wa miaka mingi katika kazi za uhandisi, manunuzi na ukandarasi (EPC) hususan katika kutekeleza miradi ya LNG duniani zimekutana na ujumbe wa Tanzania uliohudhuria kilele cha Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD7) zikionyesha nia ya kushiriki katika mradi wa ujenzi wa mitambo ya kusindika gesi asilia (LNG).

Katika kikao hicho kilichofanyika sambamba na TICAD7, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio alisema “katika kipindi cha muongo mmoja, Tanzania imepiga hatua kubwa katika sekta ya mafuta na gesi asilia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu mikubwa ya kusambaza gesi kwa ajili ya umeme, viwanda na majumbani”.

Dkt. Mataragio pia alieleza nia ya Serikali ya Tanzania kuwekeza katika utekelezaji wa mradi wa kimkakati unaokadiriwa kugharimu dola za marekani bilioni 30 na utahusisha uendelezaji wa kiasi kikubwa cha gesi asilia kilichogunduliwa katika kina kirefu cha bahari.

Dkt. Mataragio alieleza kwamba kwa sasa Serikali iko katika hatua za majadiliano ya vipengele muhimu vya mkataba wa Serikali mwenyeji (Host Government Agreemet-HGA) na kampuni za kimataifa zilizogundua gesi asilia katika kitalu namba 1, 2 na 4. Kitalu namba 1 na 4 vinaendeshwa na Kampuni ya Shell ikishirikiana na Ophir Energy na Pavilion wakati kitalu namba 2 kinaendeshwa na Kampuni ya Equinor ikishirikiana na ExxonMobil.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Chiyoda Corporation, Ndg. Ken Nagao alisema “Kwa miaka kadhaa sasa tumeshirikiana na Tanzania katika kuendeleza sekta ya gesi asilia na tunadhani tunaweza kushirikiana zaidi katika kutoa uzoefu tulionao wa zaidi ya miaka 50 katika ujenzi wa mitambo ya LNG”.

Kampuni ya Chiyoda imehusika katika ujenzi wa miradi mikubwa ya LNG ikiwemo Australia, Nigeria, Qatar na nchi nyingine nyingi ikiwa na pato ghafi la takribani Trilioni 7.2. Nae Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya JGC, Ndg. Masayuki Sato alieleza nia ya kampuni yake kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha Wananchi wake wanafaidika na rasilimali ya gesi asilia kwa kujenga mitambo ya LNG itakayowezesha uvunaji wa gesi asilia iliyogunduliwa katika kina kirefu cha bahari ya Hindi.

Akizungumza katika kikao hicho, Ndg. Sato alisema “Tumeshirikiana na Tanzania katika maandalizi ya mpango kabambe wa matumizi ya gesi asilia (NGUMP) na tusingependa kuishia hapo kwani tunadhani Tanzania ina fursa ya kuwa kituo kikubwa cha kuzalisha na kusambaza gesi asilia kwa nchi zenye mahitaji makubwa ya nishati na hivyo kukuza uchumi na pato la Taifa”.

JGC ni miongoni mwa kampuni kubwa katika ujenzi wa mitambo ya LNG na ujenzi wa miundombinu mingine katika mnyororo wa thamani wa gesi asilia, alifafanua zaidi Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa JGC.

Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga nae alieleza nia ya Wizara ya Nishati kuhakikisha gesi asilia inatumika katika kukuza uchumi wa ndani kwa kuisambaza kwa viwanda vingi zaidi ili kuchochea ajenda ya uchumi wa viwanda itakayosaidia Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

“Mpango kabambe wa matumizi ya gesi asilia unaainisha wazi kwamba tutatumia gesi yetu kusaidia kukuza uchumi na kunyanyua sekta nyingine kama vile viwanda, kilimo, uvuvi, usafirishaji na nyinginezo ili kubadilisha uchumi wa Taifa na watu wetu” alisema Mhandisi Luoga.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Rais John Magufuli wa Tanzania amesema masalia ya fikra za kikoloni walizonazo Waafrika wengi ni miongoni mwa sababu zinazofanya Bara la Afrika kushindwa kusimamia rasilimali zake ili kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akihutubia kongamano la viongozi la 2019 akisema dhana ya uhuru haiwezi kutenganishwa na kujitegemea.

“Kama hujitegemei huwezi kuwa huru, kwani uhuru wako utakuwa mikononi mwa unayemtegemea.”

“Maana hasa ya kupigania uhuru ni kurejesha rasilimali zetu na hasa rasilimali zetu, lakini pia kuwa na uamuzi kamili wa namna ya kuzisimamia na kuzitumia wa kuzitumia ili kuleta ukombozi wa kiuchumi,” amesema Rais Magufuli.

Amesema kutokana na kutoelewa dhana kamili ya uhuru, nchi za Afrika zinadhani watawala wa zamani ndiyo wenye uwezo wa kusimamia na kusaidia na kuendeleza rasilimali.

Ametaja pia sababu ya kushindwa kusimamia rasilimali na kuleta mageuzi ya kiuchumi, akisema fedha siyo msingi wa rasilimali.

“Fedha ni matokeo ya mwisho kabisa ya matumizi ya rasilimali zetu na siyo msingi wa maendeleo. Hata hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Hakutaja pesa, alijua itakuja tu kama yale tutayatimiza,” amesema.

Ametaja pia ukosefu wa ubunifu na teknolojia ya viwanda akisema Afrika haitaweza kusimamia na kutumia rasilimali zake kiuendelevu bila kuwa na viwanda.

Mbali na viwanda, ametaja kukithiri kwa migogoro na hali tete ya siasa barani Afrika akisema inasababishwa na mabeberu wanaotaka kuendelea kutumia maliasili za Afrika kwa manufaa yao.

“Wakati sisi tunapigana wao wanakula na kamwe hawatataka tuwe na amani, kwani migogoro ndiyo mtaji wao,” amesema.

Ameendelea kutaja pia tatizo la mikataba na makubaliano yanayoingiwa na wawekezaji katika kutumia rasilimali akisema, “Na hapa nchi yetu imeliwa sana kutokana na mikataba mibovu na hasa kwenye madini.”

Kuhusu uharibifu wa mazingira, Rais Magufuli amesema unasababishwa na ukataji hovyo wa msitu kwa ajili ya nishati ya majumbani kutokana na gharama kubwa za umeme na gesi asilia.

“Chanzo kingine ni uchafuzi wa mazingira unaofanywa na mataifa mengine yaliyoendelea na yenye viwanda vingi, lakini Afrika ndiyo inayoathirika zaidi a machafuko hayo,” amesema.

Akizungumzia hatua zilizochukuliwa na Serikali, Rais Magufuli amesema imetungwa sheria ya kulinda utajiri na rasilimali na maliasili ya 2017 na kupitiwa upya na kurekebisha mikataba ya uchimbaji na madini isiyo na manufaa kwa Taifa.

“Tumeweka msukumo mkubwa kwenye ujenzi wa viwanda na ukuzaji wa teknolojia ya viwanda ili mazao yanayotokana na rasilimali zetu yasindikwe kwanza kabla ya kuuzwa nje,” amesema

Alitaja pia uanzishwaji wa mradi wa bwawa la Nyerere utakaozalisha MW 2115 kwenye bonde la mto Rufiji kama njia ya kutunza mazingira, kudhibiti nidhamu za watumishi wa umma na kupamba na rushwa na ufisadi.

Wageni maarufu waliohudhuria mkutano huo walikuwa marais wastaafu kutoka baadhi ya nchi za Afrika akiwemo Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wa Tanzania.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye mkutano na wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda kwa kusikiliza kero zao na kuzitatua na kuwaagiza maofisa kilimo watembelee wakulima na kutoa elimu ya kilimo cha kisasa kuanzia ngazi ya maandalizi ya mashamba. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, akiwataka wananchi wa kijiji cha Manyada kuacha tabia ya kuharibu mazingira kwa kukata miti hovyo, huku akiagiza pia viongozi wa kijiji kujenga tabia ya kusoma mapato na matumizi.

Mtendaji wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, John Clement akisoma taarifa ya kijiji hicho, na kuelezea kuwepo na changamoto ya ukamilishwaji wa jengo la zahanati, miundombinu mibovu ya barabara, umeme, pamoja na ukosefu wa maji safi na salama hasa kutoka Ziwa Victoria.

Mwananchi John Joshua akiuliza swali kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero zao na kuzitatua na kuuliza juu ya upatikanaji wa maji safi salama hasa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria na kuondokana na matumizi ya kutumia maji yasiyo salama.

Mwananchi John Daniel akiuliza swali kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko na kuhoji juu ya fedha za ahadi za Rais John Magufuli shilingi Milioni 50 kwa kila kijiji.

Mwananchi Lukuliko Shija akiuliza swali kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko juu ya sekta ya elimu, ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule ya msingi Manyada.

Mwananchi Terezia Bundala, akiuliza swali kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, juu ya ukamilishwaji wa Zahanati ya kijiji hicho ili ipate kuwasaidia kimatibabu na kuondokana na umbali mrefu wa kufuata huduma za afya.

Diwani wa kata ya Usanda ,Mhe. Forest Nkole akijibu maswali yaliyoulizwa na wananchi kwenye mkutano huo wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Mtendaji wa Kata ya Usanda Emmanuel Maduhu akijibu swali la gharama za ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho ambalo liliulizwa na wananchi na kujibu imeshatumia fedha za Serikali Shilingi Milioni 18.5 ukitoa nguvu za wananchi na hadi kukamilika kwake zinahitajika zaidi ya Shilingi Milioni 40.

Kaimu Meneja Wakala wa Maji Safi Vijijini (RUWASA) Alfred Pesa akijibu maswali ya miradi ya maji ambayo yameulizwa na wananchi wa kijiji cha Manyada kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Dkt. Joseph Ngowi akimwakilisha Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, akijibu maswali ya idara ya afya ambayo yameulizwa na wananchi wa kijiji cha Manyada kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Msimamizi wa umeme Vijijini (REA),Helly Twaha ambaye ni  akimwakilisha meneja wa Tanesco mkoa wa Shinyanga, akijibu maswali ya umeme ambayo yameulizwa na wananchi wa kijiji cha Manyada kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

 Mkuu wa idara ya ardhi,Thomas Tukay akimwakilisha mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, akijibu maswali yaliyoulizwa na wananchi wa kijiji cha Manyada kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, pamoja na baadhi ya wataalamu,wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Awali Mtendaji wa Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Emmanuel Maduhu(kushoto) akimwelezea mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko namna wananchi walivyojitolea kujenga Zahanati ya kijiji hicho na hatua walipofikia.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akiangalia Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Manyada ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi likiwa limepasuka nyufa mara baada ya tetemeko la ardhi kupita eneo hilo,  kushoto ni Dkt. Joseph Ngowi akimwakilisha mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiwa msibani na kutoa salamu za pole kwa diwani wa Kata ya Mwamala Hamisi Masanja, ambaye amefiwa na mtoto wa kaka yake, ambapo awali ilikuwa afanye mkutano wa hadhara kwenye Kata hiyo kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua, lakini baada ya kukuta msiba ilibidi aahirishe mkutano huo na kwenda msibani.

Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, ameendelea na ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua ambapo amewaagiza maofisa kilimo kuacha tabia ya kukaa maofisini bali waanze kutembelea wakulima, na kuwapatia elimu ya kilimo cha kisasa kuanzia maandalizi ya shamba hadi mavuno.

Akizungumza wakati wa ziara yake leo Agosti 29,2019 kwenye kijiji cha Manyada kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, mkutano uliofanyika kwenye jengo la Zahanati ya kijiji hicho ameagiza maofisa kilimo wote kuacha tabia ya kukaa maofisini.

Amesema hivi sasa wakulima wanapaswa kuanza kupewa elimu ya maandalizi msimu ujao wa kilimo, kuanzia namna ya kupata mbegu bora, kuandaa mashamba, madawa mazuri ambayo watatumia, pamoja na kulima kilimo cha kisasa chenye tija, ambacho kitawapatia mavuno mengi na kuinuka kiuchumi.

“Naagiza maofisa kilimo wote wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, acheni tabia ya kukaa maofisini, bali tembeleeni wakulima na kuwapatia elimu ya kilimo cha kisasa chenye tija, kuanzia maandalizi ya shamba, pembejeo bora ambazo watazitumia hadi mavuno, ikiwa tunataka wakulima wanufaike na kilimo chao kuinuka kiuchumi,”amesema Mboneko.


“Pia nawaomba wakulima wa zao la pamba, mrudishe fedha za Pembejeo ambazo mlikopeshwa kwenye msimu wa kilimo uliopita, ili Serikali ipate fedha za kununua Pembejeo zingine ambazo zitawasaidia kwenye msimu ujao wa kilimo,”ameongeza.

Katika hatua nyingine amewapongeza wananchi wa kijiji hicho cha Manyada, kwa kujenga jengo la zahanati kwa nguvu zao wenyewe, ambalo limeshapauliwa na kuwataka wananchi waendelee kujitokeza kuchangia shughuli za maendeleo akibainisha kuwa, Serikali itawaunga mkono kukamilisha miradi hiyo.

Naye mtendaji wa kijiji cha Manyada John Clement, akisoma taarifa ya kijiji ametaja changamoto ambazo zinawakabili wananchi wa kijiji hicho kuwa ni kutokamilika ujenzi wa Zahanati, umeme wa REA kutoenea maeneo yote, pamoja na ubovu wa barabara.


Nao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho cha Manyada wamepongeza ziara hiyo ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ambayo imewapatia matumaini ya kutatuliwa kero zao, zikiwamo za miradi ya maji, barabara, umeme, elimu, pamoja na afya.
 Washiriki wa mafunzo ya kupinga mila potofu ya ukeketaji wakionesha mshikamano wa mapambano dhidi ya vitendo hivyo baada ya kuunda kamati za ulinzi wa mama na mtoto katika Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida juzi.
 Mwezeshaji wa mradi wa utetezi dhidi ya mila potofu, Japhet Kalegeya  akizungumza katika mkutano wa kuunda kamati za ulinzi wa mama na mtoto wilayani Ikungi mkoani humo.
 Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ikungi, Haroon Haroon akiwasilisha mwongozo wa ( MTAKUWA) kwa kamati za ulinzi wa mama na mototo ngazi ya Kata sita za Ikungi,Ihanja, Iglanson, Iseke,  Mhintiri  na Minyughe.
 Mwezeshaji, Daniel Saido akiwa na Mratibu wa mradi huo, Evaline Lyimo katika mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Ihanja, Sombi Majuta  akizungumza katika mkutano


 Wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
Mratibu wa mradi huo, Evaline Lyimo akizungumza katika mkutano huo.



Na Dotto Mwaibale, Singida

SHIRIKA la Foundation for Civil Society (FCS) limetoa shilingi milioni 40 kwa ajili ya mradi wa kupambana na mila potofu za ukeketaji mkoani Singida ambao umeanza mwezi Julai hadi Machi 2020. 

Fedha hizo zimetolewa kwa Shirika lisilo la kiserikali la Save the Mother and the Children of Central Tanzania (SMCCT), ambalo limeunda kamati za ulinzi wa mama na mtoto kwenye kata sita na vijiji 18 katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida kwa ajili ya mapambano hayo. 

Imeelezwa kwamba majukumu ya kamati hizo ni kumlinda mama na mtoto dhidi ya vitendo vya ukeketaji na ukatili wa kijinsia. 

Hayo yalisemwa na mwezeshaji wa mradi wa utetezi dhidi ya mila potofu, Japhet Kalegeya wilaya ni hapa juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo ambao utasaidi kupunguza vitendo hivyo au kuvimaliza kabisa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali. 

Alisema wamefikia uamuzi wa kuanzisha kamati hizo ili ziweze kuharakisha kutokomeza kabisa vitendo hivyo ambavyo vipo kinyume na haki za binadamu kama vile ukatili dhidi ya wanawake na watoto, mimba za utotoni, ndoa za utotoni ,ubakaji ,ulawiti,ukeketaji na udhalilishaji wa kijinsia katika  wilaya hiyo. 

“Mradi huu wa utetezi dhidi ya mila potofu ikiwemo ukeketaji na ukatili wa kijinsia unalenga kuwafikia wanawake na wasichana wapatao 7,200 katika wilaya ya Ikungi ambapo hali ya  unyanyasaji wa kijinsia ni mbaya”, alisema Kalegeya.

 Akitolea mfano wa hali hiyo alisema  kuanzia Januari hadi oktoba 2018 jumla ya wanafunzi 23 waliokuwa kati ya kidato cha kwanza na nne walipachikwa mimba wilayani Ikungi.

Naye mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Sekondari ya Masinda, Rosemary Seith, amelishukru na kulipongeza shirika la SMCCT kwa kushirikisha baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuwapa elimu juu ya madhara ya ukeketaji na ukatili wa kijinsia. 

“Sisi tuliohudhuria mafunzo haya yametusaidia kujua kwa mapana madhara ya vitendo hivyo vya ukeketaji na ukatili wa kijinsia sasa tunaenda kuwaelimisha na wenzetu ambao hawakubahatika kupata mafunzo haya hapa leo”, alisema. 

Mratibu wa mradi huo, Evaline Lyimo, ametaja baadhi ya malengo ya mradi huo kuwa ni kuongezeka kwa uelewa kwa jamii kuhusu kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukeketaji na kuimarisha mfumo wa utoaji wa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii hadi ifikapo Machi mwaka 2021.

Kata zilizounda kamati hizo ni lkungi, Ihanja, Iglansoni,Iseke, Minyughe na Muhintiri.