Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba (wa tatu kutoka kulia), akishirikiana na Diwani wa Kata ya Kibaigwa, Richard Kapinye, kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara wa mtandao wa 4G uliozindulliwa jana katika Mji wa Kibaigwa Wilaya ya Kongwa, Mkoani Dodoma.
Diwani wa Kata ya Kibaigwa Wilaya ya Kongwa, Mkoani Dodoma, Richard Kapinye akizungumza wakati wa uzinduzi wa rasmi wa mnara wa 4G wa kampuni ya Tigo katika eneo hilo.
Baadhi ya wakazi wa Mji wa Kibaigwa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma, walishiriki katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa huduma ya 4G ya kampuni ya mawasiliano ya Tigo.
---
Katika jitihada zake za kuboresha mawasiliano na kurahisisha maisha ya watanzania kupitia teknolojia ya kidigitali, kampuni ya mawasiliano ya Tigo, imezindua mnara wa mawasiliano wa 4G katika mji wa Kibaigwa mkoani Dodoma.

Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliohudhuriwa na wakazi wa mji huo, Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Aidan Komba, alisema uboreshaji wa mtandao kutoka 3G kwenda 4G unatarajiwa kufungua fursa mpya za kibiashara ambazo zitakuza maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo.

“Kwa kuzingatia kwamba Kibaigwa ina shughuli nyingi muhimu za kiuchumi hususani za kilimo na ufugaji na pia ni kiunganishi muhimu na maeneo mengine ya nchi, sasa ni wakati wa wakazi wa Kibaigwa na vitongoji jirani kutumia Intaneti yenye kasi zaidi ili kuendeleza biashara na shughuli mbalimbali za kiuchumi,” alisema Komba.

Uzinduzi huu unaenda sambamba na ofa maalum kwa ajili ya wateja watakaobadili laini zao kwenda mtandao wa 4G. Wateja hawa watazawadiwa kifurushi cha 4GB cha Intaneti ya bure itakayotumika ndani ya siku 7.

Vilevile, wateja watakaonunua kifurushi chochote cha intaneti kwenye mitandao uliyoboreshwa kutoka 2G kwenda 3G watazawadiwa MB100 kila wanaponunua kifurushi.

Pia kufuatia uzinduzi huu, wateja sasa wataweza kunufaika na huduma mbalimbali za kibunifu kutoka Tigo kama vile “Saizi Yako” ambayo inawapatia wateja ofa mbalimbali za SMS, Intaneti na kupiga simu kulingana na mahitaji na matumizi ya mteja. Kwa mfano mteja anayetumia dakika nyingi zaidi kuliko Intaneti na SMS atapata kifurushi cha dakika za muda wa maongezi. Mteja anayetumia zaidi Intaneti kuliko dakika za maongezi na SMS atapata kifurushi cha Intaneti kinachoendana na matumizi yake.

Tigo inaendelea kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa hususani 4G+ ili kukidhi mahitaji makubwa ya data na Intaneti yenye kasi kutokana na ongezeko la matumizi ya simu janja za bei nafuu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: