Zawadi ya picha ya kuchorwa aliyozawadiwa Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kanisa la Waadventista Wasabato la Magomeni Mwembechai katika ibada ya kuadhimisha miaka 100 tangu Kanisa hilo lianzishe idara ya familia. Mchoraji ni Sethi Samuel KENGURU, mwenye makazi yake katika jiji la Arusha.

Na Derek Murusuri, Magomeni, Dar es Salaam.


Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuheshimu uhuru wa kuabudu nchini."


Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Serikali yetu itaendelea kushirikiana na dini zote katika taifa letu ili kuleta utulivu, amani na umoja wa kitaifa. Kuja kwangu hapa katika Kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni kuabudu pamoja nanyi leo ni uthibitisho huo."


Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Kitabu cha Ayubu 22:21 kinasema, "mjue sana Mungu ili uwe na amani; ndivyo mema yatakavyokujia."

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Serikali yetu itaendelea kumtegemea Mungu katika kuwaletea watanzania maendeleo."

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Nalipongeza kanisa la Waadventista wa Sabato katika kuandaa kitabu hiki cha Tumaini la Familia."

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Kitabu hiki kitatusaidia kufundisha maadili bora."

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Nawasihi, ili kujenga familia imara itakayosaidia kuwa na taifa imara, kitabu hiki kisomwe si na waadventista wasabato peke yenu, bali waislamu na wakristo wa madhehebu mengine pia." 

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Taifa imara siku zote, msingi wake hutegemea familia imara"

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Kitabu cha Ayubu 22:21 kinasema, mjue sana Mungu ili uwe na amani. Ndivyo mema yatakavyokujia. 

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: Serikali inatambua mchango wenu muhimu katika kuhubiri neno la Mungu na kuwahudumia watanzania wote kwenye elimu, afya na maafa, bila ubaguzi.

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: Nimetiwa moyo sana kuona mnajenga Kanisa kubwa na zuri sana. Watanzania tunaweza kufanya mambo makubwa pasipo kusubiri ufadhiri wa kutoka nje.

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: Endeleeni kuwahimiza washiriki kutoa sadaka, zaka na kulipa kodi, ili kuendeleza kazi ya Mungu na vilevile kuchangia maendeleo ya taifa letu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: