Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amesema mchakato wa kusajili laini za simu kwa kuunganisha na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) usogezwe mbele hadi Desemba mwaka huu huku akiagiza Watanzania wasiokuwa na vitambulisho vya NIDA wasihukumiwe kwa laini zao kufungiwa.

Kabla ya kauli hiyo ya Rais Magufuli ambayo ameitoa leo Aprili 26,2019 akiwa mkoani Mbeya ,Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) walitangaza kuwa watazima laini za simu ambazo hazitakuwa zimesajiliwa na kuunganishwa na NIDA kwa kuweka alama ya kidole kigumba ambapo pia walitangaza kuanza kwa usajili wa laini za simu kuanzia tarehe moja ya mwezi ujao.

Akizungumza leo akiwa ziarani mkoani Mbeya pamoja na mambo mengine Rais Magufuli amezungumzia usajili wa laini za simu uliotangazwa na TCRA ambapo amesema hakuna sababu ya kuwahukumu Watanzania kwa kuzima laini zao za simu kwa kigezo kwamba hawajasajili laini za simu.

Amesema ifahamike si kwamba anazuia usajili wa laini kwani ni muhimu na usajili huo una faida zake na ni nyingi lakini amefafanua Tanzania kuna Watanzania zaidi ya milioni 50 na wenye vitambulisho vya NIDA hawafiki milioni 15.

Hivyo amesema ni vema TCRA waongeze muda wa kusajili laini za simu kwa kwenda sambamba na utoaji wa vitambulisho vya Taifa. "Watu wasihukumiwe kwa kutosajili simu kwasababu ya NIDA.Mchakato uende pamoja ili watazania wasiopata wasihukumiwe," amesema Rais Magufuli .

Amesisitiza kadri NIDA wanavyotoa vitambulisho ndivyo kasi yake iendane na usajili wa laini za simu, hivyo wasifungue laini kwa kipindi hiki kwani kufanya ni sawa na kuwahukumu Watanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: