Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Viongozi wa Mkoa wa Mtwara, wakati akikagua moja ya Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya cha Mbonde mara baada ya kukifungua Masasi mkoani Mtwara.
Sehemu ya Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya cha Mbonde mara baada ya kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Masasi mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Viongozi wa Mkoa wa Mtwara, wakati akikagua chumba cha upasuaji katika wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya cha Mbonde Masasi mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Viongozi wa Mkoa wa Mtwara akiangalia mashine ya kutoa dawa ya usingizi kkwa wagonjwa katika chumba cha upasuaji kwa wa mama wajawazito.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Mbonde mara baada ya kukifungua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Masasi mara baada ya kufungua kituo cha Afya cha Mbonde kilichopo Masasi mkoani Mtwara.
Sehemu ya wakazi wa Masasi wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akihutubia mara baada ya kufungua kituo cha afya cha Mbonde.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungua mkono wananchi hawaonekani pichani wakati akiondoka eneo la kituo cha Afya cha Mbonde. PICHA NA IKULU.
Na Fatma Salum-MAELEZO
Rais John Pombe Magufuli leo amefungua kituo cha afya cha Mbonde kilichopo wilayani Masasi mkoani Mtwara ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.
Rais Magufuli amefungua kituo hicho cha afya kwa niaba ya vituo vingine 352 vilivyojengwa kwenye maeneo mbalimbali kote nchini.
Akizungumza katika ufunguzi wa kituo hicho, Rais Magufuli amesema kuwa vituo hivyo vya afya 352 vimejengwa kwa fedha za Watanzania pamoja na wafadhili mbalimbali ambao wamekuwa wakisaidia masuala ya afya hapa nchini.
“Vituo hivi vya afya vinajumuisha hospitali za halmashauri 9, vituo vya afya 304 na zahanati 39 ambapo jumla ya gharama za ujenzi na ukarabati kwa vituo vyote ni shilingi bilioni 184,” alisema Rais Magufuli.
Amefafanua kuwa katika mkoa wa Mtwara vituo vya afya vilivyojengwa na kukarabatiwa ni 7 na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuvilinda na kuvitunza ili viendelee kuwahudumia kwa miaka mingi ijayo.
Aidha Rais Magufuli alieleza kuwa sasahivi Serikali inajenga hospitali mpya za wilaya 67 ambapo mkoani Mtwara watapata hospitali 3 katika wilaya za Masasi, Nanyamba na Mtwara.
Amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba kutoka shilingi bilioni 31 hadi bilioni 270 mwaka huu na imeajiri watumishi wa kada mbalimbali za afya wapatao 11,152 pamoja na kujenga nyumba za watumishi 306.
“Pia tumeboresha huduma za matibabu ya kibingwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwenye hospitali za rufaa za Bugando, KCMC na Mbeya ambapo watu kutoka nje ya nchi wanakuja kupata huduma hizo,” alisema Rais Magufuli.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli aliwahakikishia wananchi wa Masasi pamoja na wananchi wote wa kusini kuwa Serikali imetoa fedha nyingine shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kuwalipa wakulima wa korosho waliobaki na kuwataka kuondoa shaka kuhusu malipo yao.
Pia ameagiza wawekezaji wote waliouziwa viwanda vya kubangua korosho waanze kununua korosho na kuzibangua na kama wameshindwa wavirudishe viwanda hivyo kwa Serikali.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jafo ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imepiga hatua kubwa katika kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya afya kwani tangu nchi ipate uhuru kulikuwa na hospitali za wilaya 77 tu lakini katika kipindi hiki kifupi zinajengwa hospitali mpya 67.
Kituo cha afya cha Mbonde kilichozinduliwa leo ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 500 na kimewekwa vifaa pamoja na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 200.
Toa Maoni Yako:
0 comments: