Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amefurahishwa na kusisitiza Wabanguaji Korosho kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii na kununua vitambulisho vya Wajasiliamali wadogo kwa maslahi binafsi na ya Taifa.
Gavana Shilatu ameyasema hayo Leo Jumanne April 16, 2019 alipowatembelea Wabanguaji Korosho ndani ya Tarafa ya Mihambwe na kuwasihi maendeleo ya kweli yanapatikana kwa kujituma kwa juhudi, maarifa na nidhamu ya hali ya juu pasipo kusahau kuchukua vitambulisho vya ujasiliamali ambavyo vitawapa Kinga na imarisho la mapato yao na hivyo kupelekea kukua kiuchumi.
"Nimekuja kusikiliza na kutatua changamoto zenu. Muhimu tutambue hakuna njia ya mkato wala mteremko kwenye maendeleo zaidi ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa kwani kufanya hivyo tunamuunga mkono Rais Magufuli anayesisitiza Watanzania tuchape kazi kwa bidii. Pia tusisahau kuchukua vitambulisho vya Wajasiliamali wadogo kwani vitasaidia kuimarisha mapato binafsi na mapato ya Taifa. Makusanyo ya vitambulisho ndio hayo yanaenda kutoa Elimu bure, kujenga barabara, kuimarisha dawa na vifaa tiba hospitalini pamoja na huduma nyinginezo za kijamii na za kimaendeleo" alisisitiza Gavana Shilatu.
Katika ziara hiyo ya kuwatembelea Wajasiliamali wadogo hao, Wabanguaji Korosho Gavana Shilatu aliambatana na Mtendaji kata, Afisa Maendeleo kata na Watendaji wa Vijiji.
Toa Maoni Yako:
0 comments: