Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.

Wafanyabiashara wanaouza bidhaa mbalimbali nchini na hasa wa Jiji la Dar es Salaam wamepongeza uwepo wa huduma ya VISA katika kufanya malipo ya fedha kwa kutumia simu kwamba si tu umewafanya wawe na usalama wa fedha zao lakini kubwa zaidi imeongeza mauzo.

Wamesema kuwa mteja anapotumia huduma ya VISA katika kufanya malipo haoni shida kuchukua fedha kwenye akaunti yake na kulipia anachotoka kuliko anapoamua kulipia kwa fedha aliyonayo mkononi.

Baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema hayo jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti baada ya maofisa wa Kampuni ya VISA wa ndani na nje ya Tanzania kufanya ziara ya kuwatembelea katika maeneo ya biashara yakiwemo maduka ya nguo, vituo vya mafuta na maduka makubwa na baa ya Samaki samaki kwa lengo la kuangalia namna huduma hiyo ya VISA inavyofanya kazi na ilivyopokelewa na watoa huduma.

Kwa mujibu wa maofisa wa VISA ni kwamba biashara zaidi ya 6,000 malipo yake yanaweza kufanywa kwa kutumia huduma ya VISA ambapo kwa kutumia simu ya mkononi mteja atalipia bidhaa aliyonunua.
Mmoja ya maofisa wa Kampuni ya VISA ambao ndiyo wanaotoa huduma ya VISA kupitia simu za mkononi Henry Thuku (aliyeshika simu), akitoa maelezo machache kwa mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Puma na Wanahabari. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA - KAJUNASON/MMG.

Wakizungumza na Michuzi Blog jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti wafanyabishara hao wamesema tangu kuwepo na huduma ya kufanya malipo ya fedha kwa kutumia VISA kumeongeza mauzo yao kwani mteja anapolipia kwa VISA haoni tatizo kuchukua fedha yake iliyoko benki na kisha kulipia bidhaa aliyochukua.

"Tunao uzoefu, mteja anaponunua bidhaa na kisha akaamua kulipa kwa fedha kwa kutumia huduma ya VISA huwa haowani tabu kununua bidhaa zenye thamani ya fedha nyingi. Uzuri ni kwamba anakuwa na fedha yake benki na anapotajiwa bei anatoa fedha kutoka akaunti yake.

"Iikitokea mteja akaja na mfukoni kwake au mkono anayo Sh. 20,000 kwa mfano, ukimwabia bei ya bidhaa anayotaka na ikawa zaidi ya hapo hawezi kununua au ataomba apunguziwe lakini akitumia VISA kwake inakuwa rahisi kuingia kwenye simu yake na kuchukua fedha benki na kisha akalipa,"amesema Meneja Maendeleo wa Kampuni ya Samakisamaki Saum Wengert.

Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley na Mkurugenzi Mwandamizi wa Mauzo ya Biashara wa Kampuni ya VISA Kennedy Luhombo (mwenye tai) wakinywa Juisi pamoja na ujumbe wao mara baada ya kutembelea duka la Mak Juice lililopo Sinza, Dar es Salaam.

Amefafanua kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa wanayo hiyo huduma ya VISA na waliweka utaratibu kwa wafanyakazi ambao wataongoza kwa kuuza bidhaa zao na kisha malipo kufanywa kwa njia ya VISA wanalipwa bonasi. "Kwetu hapa anayeuza zaidi na kisha malipo kufanyika kwa VISA tunampa bonasi kama sehemu ya kumtia moyo maana fedha ikilipwa kwa mfumo huo inakuwa salama zaidi na inakwenda moja kwa moja katika akaunti ya kampuni yetu,"amesema.

Kwa upande wake Msimamizi wa Kituo cha Mafuta Puma Energy kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam Mohamed Omari (wa pili toka kushoto)  amesema VISA imerahisisha sana katika kufanya malipo kwani idadi ya wateja ambao wanalipa fedha kwa kutumia VISA imeongezeka. "Wapo wanaokuja kununua mafuta kwenye kituo chetu na malipo ya fedha wanalipa kwa kutumia huduma ya VISA.Tunawapongeza kampuni ya VISA kwa uamuzi wake wa kuleta hii huduma hiyo ambayo kwetu tunaiona ni sahihi na imekuja kwa wakati."
Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley akizungumza na mwanahabari Benard Lugongo (kushoto) wakati wakifanya ziara ya kutembelea maduka yanayotumia huduma ya VISA jijini Dar es Salaam.

Mfanyabishara wa duka la nguo JS lililopo Sinza jijini Neema Charles amesema kutokana na malipo mengi kufanyika kwa huduma ya VISA ,kumesaidia kuondoa usumbufu wa kutafuta chenji kwani mteja atatoa fedha kwenye akaunti yake ile ambayo ameambiwa tu.

Pia anasema zamani ilikuwa mteja akitajiwa bei anakwenda nje kutafuta fedha katika Tigo pesa, M-Pesa au Airtel Money ili kupata fedha ya kulipa lakini kwa sasa hakuna usumbufu kwa kutumia VISA ataingia kwenye simu yake na kufanya malipo.

Wakati huo huo Meneja wa Shoppers Plaza Maheshi Venktatesh amesema uwepo wa VISA kumesababisha uwepo wa unafuu mkubwa katika kufanya malipo kwani huchukua muda mchache na kupunguza msongamano kwa wateja.
Pia imefanya kuwe na usalama wa fedha , mteja ananunua bidhaa na kulipa kwenya akaunti moja kwa moja, hivyo hakuna hasara ambayo inaweza kujitokeza tofauti na awali kabla ya huduma hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya VIVO Energy Tanzania Limited ambayo inamiliki vituo vya mafuta vya Engen Paul Mhato (wa pili toka kulia) amesema kwa malipo ya fedha kwa kutumia VISA kumsaidia kukaa na fedha nyingi kwenye eneo la biashara."Mnapokuwa na fedha nyingi eneo la biashara usalama unakuwa mdogo na wenye tamaa ni rahisi kushawishika na kufanya uporaji wa fedha."

Meneja Biashara wa Kadi kutoka Benki ya CRDB Fadhili Mollel amewahamasisha Watanzania kutumia huduma ya VISA katika kufanya malipo mbalimbali na kwamba benki ya CRDB imetambua hilo na hivyo wenye akaunti CRDB wanayo nafasi ya kuifurahia huduma hiyo. "Maduka zaidi ya 2000 yanahudumiwa na CRDB kupitia VISA."
Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley akizungumza kulea ufafanuzi jinsi VISA inavyoweza kufanya malipo kwa haraka alipofika katika kituo cha mafuta cha Engen Msasani Dar es Salaam.
Wakizungumza baada ya kuwatembelea wafanyabiashara hao, maofisa wa Kampuni ya VISA wamesema ni jambo la faraja kuona namna ambavyo huduma hiyo imepokelewa vema na kushika kasi huku wakitumia nafasi hiyo kuwahamasisha Watanzania kuitumia VISA katika kufanya miamala ya malipo.

Pia wamesema wataendelea kutoa elimu ya kuufahamisha umma kuhusu umuhimu wa kutumia huduma ya VISA katika kufanya malipo katika simu ya mkononi ."Ni jukumu letu kuwaambia watanzania kwanini huduma hii ya VISA ni muhimu kwao,"amesema mmoja wa wakurugenzi wa VISA Henry Thuku.
Meneja Maendeleo wa Kampuni ya Samakisamaki Saum Wengert (kwanza kushoto) akieleza machache mbele ya wanahabari walitembelea kiota hicho cha maraha cha SamakiSamaki ili kujionea wateja wanavyoweza kunufaika na utumiaji wa huduma ya VISA kupitia siku ya Mkononi. Pembeni yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya VISA Afrika Mashariki Kevin Langley.

Mkurugenzi Mwandamizi wa Mauzo ya Biashara wa Kampuni ya VISA Kennedy Luhombo akitoa ufafanuzi juu ya masuala mbali mbali yanayohusu malipo kwa njia ya simu za mkononi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: