Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga ameandika machache katika ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni shukrani wa wote ambao wanaendelea kujitolea ili kuweza kuimalika kwa afya ya Mkurugenzi wa Vipindi vya Clouds Fm/TV Ruge Mtahaba (kulia).
---
Imekuwa wiki ya faraja, wiki ya kipekee kwa #FamiliaYaRugeNjeYaMutahaba.
Kwanza kabisa nimshukuru Mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye mpangaji wa yote.

Natoa shukrani za kipekee kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuonesha moyo wa upendo na ubaba kwani hakuishia kwenye mchango pekee bali amekuwa karibu na familia ya Ruge kila siku.
Asante pia kwa rafiki zetu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba pamoja na Mbunge wa Mtama Mh. Nape Nnauye ambao wamesimama mbele kabisa na kuamua kulivaa rasmi jukumu la kupambania maisha ya ndugu yangu #RugeMutahaba.

Shukrani za kipekee pia zinakwenda kwa ndugu zetu katika tasnia, Francis Antony Ciza @majizzo na #MalkiaWaNguvu, Joyce Mhavile kwa kuonesha kwamba kamwe ushindani wa kibiashara hauwezi kukata mnyororo wa undugu unaotuunganisha kama WATOTO WA TANZANIA MOJA.

Kwa upekee kabisa niseme nawashukuru sana ndugu zetu, Issa Batenga, Zamaradi, Barnaba, Mpoto na wengine wengi kwani siwezi kutaja kila mtu, lakini kwa hao wachache waliofika studio wiki hii itoshe kusema nawashukuru Watanzania wote kwa ushirikiano na kuamua kulibeba suala la Ruge.

Kwangu Ruge alishavuka viwango vya urafiki siku nyingi, kuumwa kwake kumekuwa hali ngumu kwangu. Lakini kama ilivyo 'spirit' ya Ruge mwenyewe, Moyo wangu una tumaini la kipekee kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atampa afya njema tena na atarudi katika ubora wake usio na mfano.

Mimi binafsi na taasisi yetu, inaendelea kuwa na Ruge kama tulivyofanya siku zote na tutafanya kila tulichojaaliwa kupigania afya yake.

Asanteni, tuzidi kumuombea na kushikamana.

#RugeTheFighter #RugeNiWetuSote #Clouds20
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: