Balozi wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda akitoa hotuba katika mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Galgotias
Umati wa wahitimu wa chuo kikuu cha Galgotias wakisikiliza kwa makini hotuba ya Balozi Tanzania nchini India, Baraka Luvanda.
Balozi wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda akipokea memento kutoka kwa mwanzilishi na mkuu wa chuo kikuu cha Galgotias, Bw. Suneel Galgotia.
Balozi wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu Galgotias kutunukuu vyeti kwa wahitimu wa chuo.
Balozi wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda akitoa heshima katika picha ya Mahatma Gandhi kwa kuweka shada la maua.
---
Watanzania zaidi ya 70 wakiwemo wawili wa shahada ya uzamivu wamehitumu masomo yao katika Chuo Kikuu cha Galgotias nchini India katika fani mbalimbali tarehe 14 Januari 2019.
Balozi wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya nne ya chuo hicho aliwatunuku vyeti wanafunzi hao na wengine kutoka nchi mbalimbali duniani na kuwasihi kutumia ujuzi walioupata kuchangia kikamilifu maendeleo ya nchi walizotoka.
‘Ulimwengu unasubiri uongozi mpya na mawazo mapya na kanuni na miiko madhubuti kutoka kwenu. Hivyo, kifanyeni chuo kijivune kupitia kwenu kwa kutoa michango yenye tija katika mataifa na jamii zenu, hususan kwa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na uadilifu mkubwa katika kutimiza majukumu yenu', Balozi Luvanda alisema.
Balozi Luvanda alisema kuwa wanafunzi hao wanahitimu huku dunia ikishuhudia mapinduzi ya teknolojia mbalimbali zikiwemo za kidigitali, teknolojia ya matumizi ya sarafu za kidigitali (block chain), matumizi ya kiwango kikubwa cha data katika kufanya maamuzi (big data revolution), usalama wa mitandao (cybersecurity) na matumzi ya teknolojia katika kutekeleza kazi ambazo awali zilikuwa zinafanywa na mwanadamu (artificial intelligence). Alielezea matumaini yake kuwa chuo hicho kitakuwa kimewandaa vyema wahitimu hao kukabiliana na changamoto za mapinduzi ya teknolojia katika kutekeleza majukumu yao.
Balozi alihitimisha hotuba yake kwa kuwasihi wahitimu hao kuwa, kutunukiwa vyeti sio mwisho wa kujifunza. Wanatakiwa waendelee kusoma vitabu kwa kuwa kusoma vitabu ni sawa na kuufanyia matengenzo ubungo. ‘Akili ya mwanadamu ni kama bustani, bustani isipomwagiwa maji na kupaliliwa itaota magugu na kufa kabisa. Balozi alimaliza.
Toa Maoni Yako:
0 comments: