Mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly na wapinzani wa Simba wamepata pigo baada ya beki wake Salif Coulibaly kutangaza kuachana na timu hiyo ya Misri na kutimikia Al-Shorta ya Iraq wiki hii.
Al Ahly wametangaza kuachana na beki hiyo aliyekuwa nguzo muhimu katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya AS Vita walioshinda mabao 2-0.
Miamba hiyo ya Misri ilisema wameachana na beki huyo mwenye miaka 30, ikiwa ni miezi michache tangu alipojiunga nao akitokea TP Mazembe mwaka jana.
Coulibaly alitoa mchango mkubwa wa kuisaidia Al Ahly kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2018, lakini alikuwa mmoja wa wachezaji waliolaumiwa baada ya klabu hiyo kupokea kichapo cha jumla ya mabao 4-3 kutoka kwa Esperance de Tunis baada mchezo wa kwanza kushinda 3-1.
Beki huyo wa kimataifa wa Mali alifunga mabao katika mechi za hatua ya makundi dhidi ya Township Rollers na Kampala City; alicheza dakika zote za mechi za mtoano pamoja ile Al Ahly iliyochapwa 3-0 nchini Tunisia.
Kwa ujumla, Coulibaly ameichezea Al Ahly michezo 22 tu ya mashindano yote tangu amejiunga nayo Julai mwaka jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments: