Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jeshi USU la Wanyapori na Misitu iliyofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Jeshi USU la Wanyamapori na Misitu likipita kwa ukakamavu mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa jeshi hilo zilizofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.
Jeshi USU la Wanyamapori na Misitu likionyesha picha za Viongozi wakubwa wawili Mwalimu Julius K. Nyerere (kulia) kama ishara ya mpambanaji wa kusimamia rasilimali zetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kama mtekelezaji katika kuhakikisha rasilimali zetu zinalindwa na kufaidisha Wananchi wa Tanzania na picha za wanyama zinaashiria wanyama wakubwa watano ambao ndio kivutio zaidi duniani na wamekuwa kwenye hatari ya kutoweka wakati wa sherehe za uzinduzi wa jeshi hilo zilizofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi bendera Mkurugenzi Mkuu wa Hifahi za Taifa (TANAPA), Dkt. Allan Kijazi kama ishara ya uzinduzi na kuanza kufanya kazi rasmi kwa jeshi la USU leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jeshi USU la Wanyapori na Misitu iliyofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.
---
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa wadau wote wa uhifadhi hususan jeshi letu USU kuhakikisha kuwa wanatekeza kwa azma moja nia njema ya Serikali ya kuhakikisha usalama wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori na misitu.
Makamu wa Rais ametoa rai hiyo leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jeshi Usu la Wanyamapori na Misitu iliyofanyika katika eneo la Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.
“Vilevile, nitoe rai kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya uhifadhi kuheshimu sheria za nchi, kutoa ushirikiano kwa jeshi usu na kuwa raia wema kwa kujiepusha na kuacha mara moja kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya uhifadhi ikiwemo kuingiza mifugo, kuanzisha kilimo, makazi na ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na matumizi mengineyo.” alisema Makamu wa Rais.
Utalii umekuwa moja ya vyanzo vikubwa vya kuliingizia Taifa fedha za kigeni kwa asilimia 25% na pato la Taifa kwa asilimia 17% pamoja na kutoa ajira rasmi na zisizo rasmi.
Mfumo huu mpya wa kusimamia maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori na misitu utasaidia kumaliza ujangili kabisa.
Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Nape Nnauye amesema wanatambua ukubwa wa tendo hili la uanzishwaji wa jeshi la Usu kwa faida ya nchi, kwa faida ya kizazi hiki na kizazi kijacho.
“Tunaamini kwamba pamoja na ujasiri na uzalendo lakini operesheni za jeshi hili zitafanyika kuzingatia ubinadamu ili tuwafanye wananchi waone umuhimu wa rasilimali hizi ushirikiano wao katika kuzilinda na kuzitunza ni muhimu” alisema Mwenyekiti huyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: