Mtaalamu wa magonjwa ya Damu, Vinasaba na Saratani Professa Lucio Luzatto wa Chuo cha MUHAS akifafanua jambo wakati wa semina fupi iliyokuwa na lengo la kutoa uelewa juu ya Ugonjwa wa Saratani iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni Kuli ni muongozaji wa semina hiyo Daktari Heri Tungaraza wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 
 Muongozaji wa semina hiyo Daktari Heri Tungaraza wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 
 Mtaalamu wa magonjwa ya Damu, Vinasaba na Saratani Professa Lucio Luzatto wa Chuo cha MUHAS akitilia msisitizo jambo.
 Washiriki wakifuatilia kwa makini.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
---
Mtaalamu wa magonjwa ya damu, vinasaba na saratani

Mada ilikuwa ni "Uelewa wa saratani; kutenganisha ukweli kutoka kwenye" uongo.

Professa alielezea kwa kina juu ya mada hii na kisha maswali kufuatia.

Waliojitokeza walijifunza mengi na kuahidi kuwa mabalozi wa vita dhidi ya saratani nchini Tanzania huku wakitilia mkazo hoja ya ujumbe kufika vijijini.

Saratani hapa nchini Tanzania inazidi kunyakua maisha ya ndugu zetu, marafiki na hata viongozi. Kwa mujibu wa wizara ya afya takribani watu 32,000 ugundulika na saratani kila mwaka nchini na 28,000 hufariki.

Kupambana kwa janga hilo kunahitaji ufahamu wa tatizo katika kufikia lengo hili, kulikuwa na semona ya saratani yaliyoandaliwa na Daktari Heri Tungaraza huku msemaji mkuu akiwa ni Professa Lucio Luzatto
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: