Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akitoa salamu za Wizara ya kilimo mbele ya Mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Baadhi ya wakulima wakifatilia Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) aakisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.
Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Bashiru Ally mara baada ya kuwasili kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.
Na Mathias Canal-WK, Morogoro.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Mb) ameupongeza mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 kwa kuwa dira na Muungano wenye sauti moja yenye mshikamano na mafanikio makubwa kwa wakulima nchini.
Waziri Tizeba ametoa pongezi hizo Leo tarehe 3 Octoba 2018 wakati akitoa salamu za Wizara ya kilimo mbele ya Mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA).
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Bashiri Ally, Waziri Tizeba alisema kuwa kipindi cha miaka 25 MVIWATA imekuwa mtandao wenye dhamira chanya kwa kuwaunganisha wakulima wadogo kwa kutetea maslahi yao na kujenga mikakati ya pamoja ya kujikwamua kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.
Aliitaka MVIWATA kuwa inapaswa kusimamia zaidi maslahi ya wakulima nchini kwa kuwa wahusika wakuu na wamiliki wa mfumo wa uzalishaji na kuwa sehemu ya mfumo wa maamuzi ya masuala yahusuyo maisha ya wakulima wadogo hususani mfumo wa uzalishaji na rasilimali ardhi.
Dkt Tizeba aliwahakikishia wananchama hao zaidi ya 2000 walioshiriki katika kongamano hilo la siku tatu kuwa wakulima wanapaswa kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka iwezekanavyo.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa wakulima Tanzania (MVIWATA) Ndg Stephen Ruvuga akisoma risala ya maadhimisho hayo ameipongeza serikali katika kujenga uchumi wa Taifa katika kuimarisha sekta ya kilimo nchini.
Alisema kuwa kwa kutambua hilo na hususani katika matumizi ya fedha za umma aliongeza kuwa kunapaswa kuongeza msisitizo katika usimamizi wa matumizi ya fedha za umma na kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Alisema kuwa pamoja na jitihada kubwa za serikali za kuimarisha sekta ya kilimo wakulima kwa ujumla bado wanachangamoto mbalimbali ikiwemo swala la ardhi, bei ya Mazao na soko la uhakika na mitaji ya uwezeshaji wakulima.
Toa Maoni Yako:
0 comments: