Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya Wafanyabiashara wa nchini China, leo jijini Beijing ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018 ambapo utafanyika kwa siku mbili. Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joh Pombe Magufuli, katika mkutano huo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Group, Mohamed Kiluwa ambaye ni mmoja ya baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania waliopo nchini China kuhudhuria Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya Wafanyabiashara wa nchini China,leo jijini Beijing ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018 ambapo utafanyika kwa siku mbili. Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joh Pombe Magufuli, katika mkutano huo.
Balozi wa Tanzani chini China, Mbelwa Kairuki akimtambulisha mmoja wa wafanyabiashara wa China kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Godfrey Mwambe baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzungumza nao leo jijini Beijing, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China, Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018 ambapo utafanyika kwa siku mbili.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Godfrey Mwambe akibadilishana kadi na baadhi ya Wafanyabiashara wa nchini China.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini China wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.PICHA NA MICHUZI JR-BEIJING

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inaongoza kwa kupokea uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki.

“Mtiririko wa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja nchini umeongezeka kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita na sasa wawekezaji wameipa kipaumbele Tanzania kama kitovu cha uwekezaji barani Afrika.”

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Septemba 02 ,2018) wakati akihutubia Kongamano la Biashara kati ya Tabnzania na China kwenye Hoteli ya Winstin jijini Beijing nchini China.Waziri Mkuu amesema Tanzania imethibitika kuwa ni Taifa lililodhamiria kwa dhati kujenga uchumi wa viwanda , pamoja na kulinda na kudumisha amani na utulivu.

Amesema ripoti ya uwekezaji duniani iliyotolewa mwaka 2018, inaonesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kupokea uwekezaji katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na imepokea kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.2 mwaka 2017.Waziri Mkuu amesema Tanzania inafanya juhudi kubwa ili iweze kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, hivyo imeweka mkazo mkubwa katika kujenga msingi imara wa viwanda.

“Ili kufanikisha hilo tumeandaa Ukanda wa Kuzalisha kwa ajili ya mauzo ya Nje na Ukanda maalum wa Kiuchumi tukilenga kutimiza mkakakati wetu wa kukuza uchumi wa viwanda na biashara.”Akizungumzia kuhusu sekta ya fedha, Waziri Mkuu amesema Tanzania inawakaribisha wawekezaji kuanzisha Taasisi za Kifedha kama vile benki kwa ajili ya kutoa mikopo midogo midogo, benki za uwekezaji, benki za kilimo na benki za biashara.

Kuhusu uwekezaji kutoka China uliosajiliwa na Kituio cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kati ya Novemba 2015 hadi Oktoba 2017, Waziri Mkuu amesema umefikia thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.077 na umejikita katika meneo ya kilimo, majengo ya biashara, rasilimali watu, viwanda na utalii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: