Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia zoezi la utiaji saini Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd na KTMI Co ltd.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika Bandari ya Mwanza Kusini mara baada ya kushudia utiaji saini wa Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd na KTMI Co ltd.
Mfano wa Meli mpya itakayojengwa ambayo Mkataba wake umesainiwa. Meli hiyo itakuwa na Urefu wa Mita 90, Kimo mita 10, uwezo wa kubeba abiria 1200 magari madogo 20, mizigo tani 400 na itakuwa ikisafiri kwa muda wa masaa sita tu kutoka Mwanza mpaka mkoa wa Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Song Geum Yong watatu kutoka kushoto waliokaa,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella wakwanza kulia waliokaa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe watatu kutoka kulia pamoja na wabunge mbalimbali wa mikoa ya Kanda ya ziwa. PICHA NA IKULU.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: