Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar as Salaam wakati wa Semina jinsi ya kurepot Kuhusu ugonjwa wa Ebola na namna ya kuzuia usiingie nchini.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii).
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Adiele Onyeze Akizungumza na waandishi wa habari kuhusukushirikiana na Tanzania katika kuzuia milipuko ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa huo wa Ebola ambao umekuwa ukiripotiwa mara kwa mara katika nchi za Afrika leo katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari Washiriki wakifuatilia semina hiyo juu ya uelewa wa ugonjwa Ebola
Waandishi wa Habari wametakiwa kushirikiana na Serikali katika kuihabarisha jamii ili kuepukana na janga hatari la ugonjwa wa Ebola.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameyabainisha hayo wakati wa kufungua mafunzo maalum kwa waandishi wa namna ya kutoa taarifa za ugonjwa huo wa Ebola.
Jamii imetakiwa kujua dalili za ugonjwa huo wa Ebola kwa kina kwani kupitia Wanahabari,mafunzo hayo yatasaidia sana kutoa elimu na itaenea maeneo mengi.
“Ugonjwa huu wa Ebola kiukweli ni ugonjwa hatari. Na tokea kutokea katika nchi za wenzetu umesababisha madhara makubwa sana ikiwemo Uchumi ikiwemo masuala ya biashara na uwekezaji.
Imebainishwa kuwa madhara ya kiuchumi juu ya Ebola yangeuwa watu wengi zaidi kuliko ugonjwa wenyewe. Sisi tulikuwa na wasiwasi sana ndio maana tulienda wenyewe huko kufuatilia..mimi nilienda mipakani Rusumo na Mganga Mkuu yeye alienda mipaka ya Ngala na maeneo mengine.” Amesema Waziri Ummy Mwalimu.
Na kuongeza kuwa, tatizo kubwa ni suala la wasafiri wanaopita njia za panya kwani zimekuwa zikiwapa changamoto na wameomba Kamati za Ulinzi na Usalama kuhakikisha wanalinda maeneo hayo.
Lakini nataka kukiri kwa kweli baadhi ya mipaka hali sio nzuri. wameweka tenti pekee bila mahitaji mengine ikiwemo sehemu za Choo. kiukweli tumejiandaa ila kuna maeneo tunahitaji kuyaboresha” alifafanua Waziri Ummy Mwalimu.
Hata Waziri amebainisha kuwa, wamejipanga na wanaendelea kuona njia bora zaidi mara kwa mara ambapo wameomba Wanahabari kushirikiana na Wizara kupata taarifa na uelewa zaidi.
“Ndugu wanahabari kupitia semina hii itaongeza uelewa wa ugonjwa wa Ebola. Nimefurahi sana Wanahabari na wachora vibonzo wameanza kutoa taarifa na kuchora vibonzo juu ya ebola.
Nimalizie kwa kusema tena ..Hadi saa hakuna mgonjwa yeyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa na Virusi
vya Ebola hapa Nchini. Hata hivyo kutokana na ukweli kwamba kuna mwingiliano mkubwa wa wananchi kati ya nchi hizi mbili na ugonjwa huu kugunduliwa kwenye jimbo la Kivu Kaskazini ambalo linapakana na nchi ya
Uganda ni ukweli unaotuweka kwenye hali ya wasiwasi mkubwa” Alimalizia Waziri Ummy Mwalimu.
Waziri pia aliwashukuru Shirika la Afya (WHO) kwa kuweza kuisaidia mapambano dhidi ya Ebola kwa kuwezesha fedha za manunuzi ya madawa na kutoa elimu.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Adiele Onyeze amebainisha kuwa wataendelea kushirikiana na Tanzania katika kuzuia milipuko ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa huo wa Ebola ambao umekuwa ukiripotiwa mara kwa mara katika nchi za Afrika.
“Dunia kwa sasa ipo katika mapambano ya kuzuia milipuko ya magonjwa. Sisi WHO tumejipanga kusaidia juhudi za Mataifa yote yenye hatari hivyo tutasaidia kutoa elimu na uwelewa kwa Wananchi wote” alieleza Dkt. Adiele Onyeze.
Toa Maoni Yako:
0 comments: