Wengi wetu tunapenda kula ugali wa dona kwani una virutubisho kuliko sembe.
Hata hivyo wengi hatujui hatari ya kula ugali huo kiafya. Mahindi hushambuliwa na vimelea tofauti ikiwemo ukungu (fangasi) ambao baadhi yake hutoa sumu ziitwazo sumukuvu.
Mahindi ndio zao linaloshambuliwa zaidi na sumukuvu na kwa Tanzania takribani moja ya tatu ya mahindi yanapovunwa tu huwa yamesheheni sumukuvu
Sumukuvu husababisha kansa hususani kansa ya ini na ya koo na matatizo mengine hasa kwa watoto.
Fangasi wanaoshambulia mahindi na kutoa sumukuvu hukua zaidi chini ya ngozi ya punje ya hindi. Mahindi yakikobolewa, sehemu kubwa ya fangasi hawa na sumu zake huondoka na pumba. Kwa hiyo mahindi yakikobolewa, yakaoshwa kisha kusagwa unga huwa na kiwango kidogo zaidi cha sumukuvu kuliko mahindi yakisagwa hivyo hivyo.
Kwa hiyo, kama wewe ni mpenzi wa dona, hakikisha mahindi umeyachambua na kuyaosha kabla ya kuyasaga.
Epuka kula dona ambalo hujui mahindi yake yaliandaliwaje kwanza.
Kumbuka, wafanyabiashara wasio waaminifu huandaa unga bila kuosha mahindi na mara nyingine mahindi hayo huwa yaliwekwa dawa za kuua wadudu ghalani.
Zamani watu walikula dona, madhara pengine hayakuwa makubwa. Hii ni kwa sababu lifestyle ya zamani ilikuwa tofauti, watu wakila vyakula vya asili zaidi.
Kwa lifestyle tunazoishi sasa, ni wazi kwamba kuwa exposed kwa risks kama hizi huongeza hatari ya kuathirika.
JILINDE NA ILINDE FAMILIA YAKO.
Toa Maoni Yako:
0 comments: