Wiki hii TatuMzuka imezindua jackpot ya Jumatano ikiwa ni jackpot ya pili ndani ya wiki moja. Watanzania sasa watapata fursa ya kuwa washindi wa jackpots mara mbili na hivyo kutengeneza washindi wengi zaidi kupitia jackpots.

Jackpot ya jumatano ambayo itahusisha wachezaji wote waliocheza tangu jumapili itakuwa inaonyeshwa saa 3 usiku kupitia Clouds TV na EATV.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Bwana Sebastian Maganga alisema kampuni ya The Network ambao ni wamiliki wa mchezo wa namba wa TatuMzuka imekuwa ikiangalia namna ya kuongeza nafasi za Watanzania kushinda kwa wingi na kwa kiasi ambacho kinabadilisha maisha yao.

“Tangu tulipoanza mwaka mmoja uliopita tumetoa jackpot ya kihistoria ya milioni 300, na sasa kwa kuongeza jackpot ya jumatano watanzania hawatahitaji kusubiri wiki nzima kushinda, itakuwa sasa jumatano na jumapili” Alisisitiza Maganga

Baada ya uzinduzi huu, Tatumzuka sasa itaondoa jackpot ya kila siku ya Mzuka Deile na kuibadilisha na droo za vipindi maalumu ndani ya siku moja. Droo hizi zitatengeneza mamilionea wengi kwa haraka na kuufanya TatuMzuka kuwa mchezo unaotengeneza mamilionea wengi zaidi kuliko mchezo mwingine katika soko.
Akiongea wakati wa uzinduzi, balozi wa TatuMzuka Mussa Hussein (pichani) alisema hii ni fursa kubwa kwa watanzania kubadili maisha yao kupitia jackpots mbili kubwa kila wiki.

“Kwa tiketi moja ya shilingi 500 sasa Watanzania watakuwa wanasubiri kwa siku 3 tu kushinda kupitia jackpot za jumatano na jumapili. Hii itakata kiu ya wachezaji wetu wapendwa ya kusubiri muda mrefu kushinda kiasi kikubwa” Aliongeza Hussein

Ili kuongeza nafasi ya watanzania wengi kutazama shoo za jackpots Bwana Maganga alisisitiza kwamba The Network imeiongeza TBC1 kati ya vituo vitakavyokuwa vinaonyesha mubashara shoo ya jackpot ya jumapili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: