Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa DAWASA (Picha za chini) katika ufunguzi wa mradi wa maji Kiwalani Bom Bom jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna- Kajunason/MMG.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza machache na kumkaribisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, kuzungumza wananchi wa Kiwalani Bom Bom leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi na wananchi wakifuatilia kwa makini.
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa akitoa shukrani zake kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa na uongozi wa DAWASA kwa kuweza kuwawekea mradi wa maji Kiwalani Bom Bom jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mradi wa Kiwalani Mhandisi Ramadhani Mtindasi amesema kuwa mradi wa Kiwalani ni Km 13.32 ukiwa na vizimba vinane lakini mpaka sasa tayari wameshajenga vizimba vitano na karibuni watamalizia vitatu. Mapema leo katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa (wannekushoto) kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (watatu kushoto) wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa mradi wa maji Kiwalani Bom Bom jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa (kulia) kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (kushoto) wakifungua maji kuashiria ufunguzi wa mradi wa maji Kiwalani Bom Bom jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akiwa amebeba ndoo ya maji kumtua mama ikiwa ni ishara ya kuonyesha jinsi walivyowatua ndoo akina mama wa Kiwalani Bom Bom jijini Dar es Salaam.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amesema lengo la Serikali ni kuona ifikapo mwaka 2020 upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es Salaam unafika asilimia 95.
Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akihutubia wananchi katika hafla ya kuzindua mradi wa maji katika Kata ya Kiwalani jijini Dar es Salaam unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA).
Profesa Mbarawa amesema, kumalizika kwa mradi huu ni moja ya ahadi ya serikali ya kuhakikisha kila mwananchi na eneo la Kiwalani wana zaidi ya miaka 30 hawajawahi kuwa na maji safi ya Dawasa na wamekuwa wanatumia chumvi katika kipindi chote hicho.
Amesema Profesa Mbarawa, ukiachana na mradi huo mpaka sasa serikali bado ina miradi mingine ikiwamo mradi wa Bilioni 133.2 ambao ni mradi wa kutoka Benki ya dunia na maji yatakayozalishwa hapo yatapatikana maeneo ya Dar es Salaam na Bagamoyo.
Amesema, Mradi mwingine ni wa Usambazaji maji wa Kiluvya, Salasala, Kimara na Goba utakaogharimu Bil 74.46, huku akisisitiza zaidi katika miradi ukiwamo mradi wa maji taka wenye thamani ya Bil 156.64 ambao yote kwa amoja ikikamilika itahakikisha inaleta manufaa kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani.
"Kwa sasa tupo asilimia 75, lakini asilimia 95 inawezekana kabisa, hivyo niwahakikishie wananchi kuwa miradi hii tutaipeleka katika maeneo mengine hasa yaliyopo kusini mwa jiji hilo," amesema.
Amesema kupitia mradi huo, Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), watapata mapato ambayo yatawawezesha kufanya miradi mingi ya kuwaunganishia wananchi maji kuliko kuitegemea Serikali.
"Mamlaka hii ina uwezo wa kufanya miradi mbalimbali bila kutegemea Serikali, kipindi cha nyuma ilisinzia kidogo lakini naamini kwa uongozi huu mpya kasi ya mapato itaongezeka," amesema.
Kwa upande wake, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja amesema katika jiji hilo maeneo yenye changamoto ya maji ni pamoja na Gongo la mboto, Kiwalani na Kigamboni.
Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa miradi yote itakapokamilika wakazi wa Dar es Salaam na Pwani watapata maji ya uhakika.
Luhemeja amesema kuwa, ndani ya siku 100 za DAWASA Mpya watahakikisha miradi inakamilika na mingine wakandarasi wakiingia kazini ili kufanikisha upatikanaji wa maji kwa wakazi wote na wakitimiza hitaji la kuongeza wateja wapya 200,000 kutokana na miradi hiyo ya maji.
Pamoja na hilo, Luhemeja amesema kuwa moja ya mkakati mwingine wa DAWASAmya ni kuona wanaongeza ukusanyaji wa mapato kwa kufikia Bilioni 12 ikiwamo kuwafuatilia wale wote wenye madeni.
Mradi huo uliogharimu Sh258 milioni utanufaisha wananchi wa kata ya Kiwalani ambao wataunganishiwa maji kwa gharama nafuu lakini pia kwa wale wasio na uwezo watachota maji kwenye vioksi ambavyo vitajengwa na DAWASA.
Toa Maoni Yako:
0 comments: