Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua hali ya uhifadhi wa mahindi na kubaini akiba ya chakula mara baada ya kutembelea Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea leo Tarehe 4 Agosti 2018.
Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akijadili jambo na Mratibu wa mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa Mhandisi Imani Nzobonaliba baada ya kutembelea Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea leo Tarehe 4 Agosti 2018.
Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akijadili jambo wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa katika ofisi ya Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea leo Tarehe 4 Agosti 2018.
Na Mathias Canal, WK-Ruvuma.
Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameupongeza uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa kasi ya utekelezaji Wa ujenzi wa mradi wa maghala na Vihenge vya kisasa.
Mhandisi Mtigumwe ametoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi ujenzi wa mradi huo leo Tarehe 4 Agosti 2018 katika kanda ya wakala Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ambapo alitaja maeneo yatakayojengwa mradi huo kuwa ni pamoja na Wilaya ya Dodoma Mkoani Dodoma, Mpanda (Katavi), Songea (Ruvuma), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe), Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga Mjini (Shinyanga), na Babati (Manyara).
Mradi huo ni matokeo ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland kusaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula
Alisema wizara ya kilimo imeingia katika ujenzi huo wa maghala na vihenge vya kisasa ambao utaongeza uwezo wa kuhifadhi mahindi kutoka Tani 251,000 za sasa hadi Tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inahitaji watumishi wachapa kazi na kwamba wananchi na jamii kwa ujumla wake inategemea hifadhi ya chakula kilichohifadhiwa na NFRA pindi inapotokea kadhia ya ukosefu au upungufu wa chakula.
Akikagua mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa, Mtigumwe alijionea jinsi mkandarasi kutoka kampuni ya Ferum ya nchini Poland anavyoendelea na ujenzi na ujenzi ili kukamilisha kwa wakati kwa mujibu wa makubaliano.
Katibu Mkuu huyo alimemsihi mkandarasi kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili kumaliza kazi hiyo mwezi Desemba mwakani kwa mujibu wa mkataba.
Pia, alitoa msisitizo kwamba kwa kuwa teknolojia ya ujenzi wa vihenge vya kisasa ni ngeni nchini, atawasiliana na Bodi ya wakandarasi (Engineers Registration Board-ERB) ili kuweza kupatiwa Wahandisi vijana watakaokuwa wakihusika moja kwa moja katika mradi huo kwa ajili ya kujifunza na kubakisha utaalamu huo nyumbani Tanzania.
Mhandisi Mtigumwe amefanya mazungumzo na watumishi wa NFRA Kanda ya Makambako ambapo aliwasisitiza kufanya kazi kwa weledi mkubwa, nidhamu na utumishi uliotukuka.
Mikataba ya ujenzi ilianza kufanya kazi tarehe 9 Disemba 2017 ambapo Mradi huo utatekelezwa na kampuni mbili za Kandarasi kutoka Poland ambazo ni (Feerum S.A na Unia Araj Realizacje Sp.o.o) ambapo msimamizi wa utekelezaji wa mradi ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na kuhusisha ujenzi wa vihenge vya kisasa, maghala ya kisasa pamoja na ukarabati wa ofisi.
Mhandisi Mtigumwe amefanya ziara ya siku moja Mkoani Ruvuma akiwa safarini kuelekea Mkoani Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki kilele cha maadhimisho ya maonesho ya wakulima MKoani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: