Nakumbuka niliwahi kuongea mwanzoni sanaa juu ya ile hamahama ya kwanza nikasema hii hama hama ni matokeo ya kuwapokea wageni na kuwakaribisha hadi chumbani na kuwasahau wenyeji.

Chadema ilijengwa sanaa katika suala la viongozi vijana walipikwa watu kama kina Halima Mdee, John Mnyika kina Heche hawakufika tu chadema na kupewa nafasi za kugombea ni vijana ambao waliandaliwa kwa mda kuja kuwa viongozi. Japo inaweza ikawa sio kwa muda mreeefu sana ila walipikwa, waliandaliwa na walifundishwa namna ya kukipigania chama na kupigania haki za wananchi na Hata kukipigania chama Hata kusimama pamoja kwenye misukosuko.

Lakini kwanzia 2015 taswira nzima ya chadema ilibadilika kama kauli mbiu ilivyokuwa ikisema NI WAKATI WA MABADILIKO. Mabadiliko haya yalikuwa na maana pana sana na mm Leo nidhubutu kusema tu haikuwa tu kubadilisha utawala ama kuing'oa ccm Bali mabadiliko yalienda mbali sana Hata chadema kusahau misingi yao ya kupata viongozi wenye uwezo wa kusimamia chama na kukipigania, tulishuhudia wageni wengi wakipewa nafasi kwa kuangalia upepo tu wa ushindi bila kuangalia adhari za baadae.

Tuliangalia ushindi, tuliangalia kupata wabunge wengi zaidi wa upinzani hatukuangalia aina ya viongozi ambao tunawaweka kupata ushindi.

Hatukuangalia wageni walikuja kwa upepo gani na labda hatukufikiri ipo siku upepo huu utaisha kama sio kuondoka kabisa.

Tuliwaamini, tukawapa nafasi na haya ndio matokeo ya kuwaamini sana wageni kuliko wazawa ambao walifinyangwa na kufunzwa katika misingi bora ya uongozi.

Chadema lazima tukili tulikosea sanaa na tuliwakosea sana wananchi kuwapelekea watu ambao hawakuwa machaguo ya chama toka awali Bali machaguo ya mabadiliko katika chama.

Leo kila kukicha watu wanahama wengine tuliwaamini sana na chama wengine tuliwapa nafasi tu sababu wakiletee ushindi chama tukatoka katika misingi yetu ya kuwaandaa vijana kuja kukipigania chama na kuwa viongozi bora.

Ni makosa makubwa tuliyafanya tena makubwa sana japo najua chadema hawataki kukili hili.

Haya ndio matokeo ya mabadiliko haya ndio matokeo ya kutaka ushindi mkubwa bila kijali athari za big result now.

Chadema tulikosea hasa viongozi walitukosea sana ... Acha tupite katika moto huu na tujifunze na tuelewe binadamu sio wa kumwamini kirahisi rahisi.

Na labda tu SAA nyingine itufunze na kuturudisha katika misingi yetu ya chama.

Neema Godfrey Tz.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: