Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akiwa katika kikao na uongozi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma, wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akizungumza na mmoja wa Wakurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma, Bibi. Catherine Mwimbe wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kushoto) akizungumza na Wakurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma mara alipokamilisha ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
Jengo la Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma likiwa limekamilika ambapo hapo baadaye kitakuwa kikitengeneza vinywaji mbalimbali yakiwemo maji ya kunywa yatayopewa jina la “Asante”.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akiwa pamoja na viongozi wengine wa TRA wakitazama shamba la mizabibu ambalo ni mali ya Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma, Bibi. Catherine Mwimbe wakitazama miundimbinu ya kiwandani hapo wakati wa ziara yake ya kikazi kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia), Kaimu Kamishna wa Walipakodi Wakubwa wa TRA, Bw. Alfred Mregi (kushoto) wakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma, wakiwa katika mazungumza ndani ya kiwanda hicho wakati wa ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA).
NA RACHEL MKUNDAI, DODOMA.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere, amewataka wafanyabiashara wote nchini ambao wanakutana na changamoto za kikodi kuwasiliana na ofisi za TRA zilizo karibu nao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Kamishna Kichere ameyasema hayo alipotembelea kiwanda wa DI&PC kinachotengeneza vinywaji kilichopo jijini Dodoma na kuongeza kuwa TRA ipo tayari kusikiliza changamoto zozote za kikodi kutoka kwa wafanyabiashara na itazifanyia kazi kwa kushirikiana na wafanyabiashara hao ili kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato na wafanyabiashara wanalipa kodi zao kwa wakati.
“Wafanyabiashara wale wenye changamoto za kikodi waje, tukae tuongee nao, na tuone namna ya kuzishughulikia na wafanyabiashara walipe kodi kwa wakati, tusonge mbele”, ameongeza Kamishna Mkuu wa TRA”, amesema Kamisha Kichere
Naye mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda hicho Katherine Mwimbe, amesema ujio wa Kamishna Mkuu wa TRA katika kiwanda hicho umeleta faraja kwao kwa sababu wamepata fursa ya kuwasilisha kwake moja kwa moja changamoto za kikodi walizokuwa nazo na Kamishna amewahakikishia kuzifanyia kazi haraka.
Aidha, Mwimbe ameshukuru serikali pamoja na TRA kwa kupitia marekebisho ya sheria na kuweza kutoa msamaha wa madeni ya riba na faini za kodi za nyuma kwa wafanyabiashara kitu ambacho kilikuwa ni kilio cha wafanyabiashara wengi.
“Kwa kweli nimefurahishwa sana na hatua ya Kamishna Mkuu wa TRA kufuta madeni ya riba na faini katika madeni ya kodi za miaka ya nyuma na niwasihi wafanyabiashara wenzangu kutumia fursa hii vizuri na kulipa kodi kwa wakati”, amesema
Katika kikao chake kilichomalizika hivi karibuni jijini Dodoma, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limefanyia marekebisho sheria ya kodi ya mwaka 2015 na kusamehe madeni ya riba na faini katika kodi za nyuma ambapo walipakodi watatakiwa kulipa kodi zao za msingi katika muda wa mwaka wa fedha 2018/2019.
Hata hivyo, msamaha huu unajumuisha kodi zote zinazosimamiwa na TRA kama ilivyoainishwa katika sheria ya fedha ya mwaka 2018 na ila hautahusu sheria zinazosimamiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo sheria ya Forodha.
Pamoja na hayo kutakuwepo na vigezo maalumu kwa watakaonufaika na msamaha huo ambapo watatakiwa kuwasilisha maombi ya msamaha kwa kujaza fomu maalumu Na. ITX207.01.E inayopatikana katika toviti ya TRA ikiambatana na maelezo ya kuonesha kiasi anachodaiwa pamoja kukubali kwa hiyari kulipa deni lake la msingi Yaani Principal Tax.
Toa Maoni Yako:
0 comments: