Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege hiyo mpya na yakisasa aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmoja wa Marubani aliyekuja na ndege hiyo (haonekani pichani )mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali ikitua katika Ardhi ya Tanzania wakati ikitokea nchini Marekani.
Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali ikipewa Heshma ya kumwagiwa maji (Water salute ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali ikiwasili katika uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
*Rais Magufuli akabidhiwa, aipokea kwa kukata utepe
*Imetua katika ardhi ya Tanzania saa 11:25 jioni, nderemo zatawala
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
RAIS Dk.John Magufuli amewaongoza viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na Watanzania kupokea ndege mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 262 aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ambayo imetua katika ardhi ya Tanzania saa 11.25 jioni.
Ndege hiyo kabla ya kutua ilichukua dakika kadhaa ikionekana katika anga la Tanzania huku Rais Magufuli na Watanzania kwa ujumla wakiishangilia wakati inashuka.
Mbali na Rais Magufuli pia alikuwepo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan , Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali. Baada ya ndege hiyo kutua ilipata heshima ya kumwagiwa maji kama ishara ya kuipokea rasmi.
Ndege hiyo ambayo ni kubwa na ya kisasa baada ya kupata heshima ya kumwagiwa maji kama ishara ya kuikaribisha ilikwenda eneo maalumu ambalo Rais amewaongoza Watanzania wengine kuipokea.
Baada ya ndege hiyo kusimama rasmi ulifunguliwa mlango ili waliokuja nayo washuke ambapo mlango ulifunguliwa saa 11:38 ambapo marubani walioleta ndege walikuwa wa kwanza kushuka huku wakipunga mkono.
Rais Magufuli aliipokea ndege hiyo kwa kukata maalumu kama kiashirio cha kuipokea rasmi ndege hiyo.
Hivyo waliokuja na ndege hiyo waliikabidhi kwa Rais ambapo alikatata utepe huo kushiaria kuipokea.
Rais Magufuli baada ya kuipokea aliingia ndani ya ndege hiyo. Rais Magufuli amesema kuwa ujio ndege ni heshima na ni mali ya Watanzania na kuwataka wananchi watangulize maslahi ya Tanzania na kwamba tabia ya wizi, dhuluma haina nafasi na wengi.
Amesema hapo zamani katika shirika hilo kulikuwa na mambo ambayo hayakuwa na maana na ndio maana ndege hizo ni mali ya Serikali na ATCL wamekodishiwa.
“Tumeona mkono wa Serikali uingie ili kila kinachoingia tukione.Watanzania wengi wanaunga mkono na wale wachache ambao hawaungi mkono Mungu atawaumbua,”amesema Rais Magufuli.
Kwa upande wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya ndege hiyo amesema ni fahari kubwa kwani ni mali ya Watanzania.
Amesema wakati Rais anahimiza watu kubana matumizi wengi walikuwa hawamuelewi lakini sasa wanaona yanayofanyika.
Wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ndani ya ndege hiyo amesema Rais anayo nia ya dhati ya kuleta maendeleo na kwamba kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu imesababisha ujio wa ndege hiyo.
“Rais anahimiza watu kufanya kazi na matoke yake watu wanafanya kazi na kulipa kodi ambayo ndio imesababisha kununulwa kwa ndege hiyo na nyingine,”amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments: