Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano wa mabaara kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji yaliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa mkutano huo, Dkt. Lorah Madete akitoa neno la ufunguzi wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Dr. Idda Swai akiwsailisha utafiti juu ya uhusiano kati ya Serikali kuu na serikali za mitaa na athari zake katika kutoa huduma kwa wananchi wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab) kutoka ESRF, Mussa Martine akiwasilisha mada kuhusu huduma za tafiti za kifedha kwenye miji wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mtafiti Mshiriki kutoka Taasisi inayoshughulikia makazi ya watu katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Dr Nathalie Jean-Baptiste akiwasilisha mada kuhusu utafiti uliofanywa wa maisha ya kila siku ya wananchi kwenye miji ya Tanzania wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Bw. Anton Cartwright kutoka Taasisi ya Miji ya Afrika iliyopo Afrika Kusini, akielezea mipangilio ya programu hiyo kuelekea mabadiliko ya miji iliyopangwa wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida (kushoto) na Mwenyekiti wa mkutano huo, Dkt. Lorah Madete wakijadiliana jambo wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mtafiti Mwandamizi wa ESRF, Prof. Haidari Amani akifafanua jambo wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya washiriki wakichangia mada zilizowasilishwa wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Washiriki wakiwa kwenye vikundi kazi wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Msechu Traditional Band wakitoa burudani ya kuhamasisha mipango miji salama na makazi bora wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu,
WATAFITI waliokuwa wakifanyia utafiti mada kuhusu ukuaji bora wa miji nchini Tanzania, wamekamilisha kazi hiyo na kuwasilisha katika mkutano mkubwa wa wadau chini ya mwavuli wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) siku ya Ijumaa tarehe 8 Juni 2018.
Katika mkutano huo ambao ulifunguliwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida, ilielezwa kuwa Tanzania Urbanisation Laboratory (TULab)  ilikuwa na mafanikio makubwa kutokana na kuonesha njia bora ya ukuaji wa miji nchini Tanzania kwa kuzingatia uchumi wa viwanda katika tafiti zake tatu.
TULab ilibuniwa mwaka jana kufuatia uchambuzi wa hoja ya Better Urban Growth in Tanzania ambayo ilijengwa katika kuhakikisha kunakuwepo na uelewa na kuuchochea mazungumzo ya kisera juu ya mabadiliko muhimu yanayotarajiwa katika kuelekea nchi yenye majiji makubwa yanayoshindana.
Mkutano wa mwishoni wa wiki uliitishwa kwa ajili ya kuona kilichojiri katika tafiti tatu kabla ya utafiti mwingine wa nne kufanyika, baadae mwaka huu.
Utafiti huo umelenga kutoa majibu kwa maswali yanayohusu maendeleo ya miji nchini Tanzania ambapo wadau wanatakiwa kuona.
Dkt.  Kida alishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa kukubali kuwa mwenyekiti wa jukwaa hilo lenye umuhimu kwa maendeleo ya taifa.
Septemba mwaka jana kulianzishwa tafiti tatu ambazo zilichangiwa vyema na wajumbe na sasa mkutano huo ulikuwa unatoa taarifa za mwisho kuhusu nini wamekibaini katika tafiti hizo tatu.
Utafiti wa kwanza ulilenga kuelewa ugharimiaji wa miundombinu na huduma katika majiji makubwa 6 nchini Tanzania. Utafiti wa pili ulichunguza uhusiano kati ya serikali kuu na serikali za mitaa na namna uhusiano huo unavyo athiri ugharamiaji wa miundombinu na utoaji wa huduma katika miji, na utafiti wa tatu ulilenga kuibua taarifa na takwimu ambazo zilikuwa hazijabainika hasa katika masuala ya maji.
Tafiti zote hizo kwa mujibu wa Dkt. Kida zitasaidia kuandaa mwongozo wa kuipeleka Tanzania katika ukuaji bora wa miji. Alisema kwamba mwongozo huo utatoa tafakari ya ndani zaidi kuhusu sera na vionjo muhimu vya maendeleo na changamoto zake.
Aidha akifafanua zaidi alisema kwamba TULab katika miezi michache ijayo itafanya utafiti mwingine kuhusu uhusiano wa ukuaji wa miji na  viwanda na pia itaendesha shindano la mawazo yenye ubunifu katika kuboresha miji.
 Na kwamba kutakuwa na mkutano mwingine Septemba 14, 2018 kabla ya kuzindua mdogo wa mwongozo wa ukuaji wa miji Novemba mwaka huu. Uzinduzi mkubwa wa Mwongozo huo kitaifa inatajiwa kuwa Julai 19, 2019.
Dkt. Kida alisema tafiti zote zinatarajiwa kuisadia serikali katika kufanikisha mipango ya uratibu wa miji ambayo inakuwa kwa kasi sana huku Dar es salaam ukiwa mji wa pili duniani kukua kwa kasi kubwa.
Wakiwasilisha tafiti zao wamesema kwamba bila kuongezeka kwa makusanyo ya maduhuli kutokana na vyanzo vya halmashauri zenyewe na vyanzo vingine vya mapato kwa ajili ya miradi ya maendeoleo kutakuwa na shida kubwa katika kuwa na miji  iliyoratibiwa nzuri.
Aidha ilielezwa ipo haja ya sekta binafsi na umma kushirikiana katika kuhakikisha kwamba fedha zinaozhitajika kwa ajili ya maendeleo ya miji zinapatikana .
Watafiti pia walisema kutokana na kasi iliyopo ni shida kubwa kwa halmashauri na miji kuweza kuwa na utaratibu bora.
Naye Bw. Anton Cartwright alisema kutokana na kukua kwa miji ipo haja ya wadau kushirikiana katika kuhakikisha kwamba miji inakua kwa utaratibu kwa kuwa kukua ni lazima ikue.
Pamoja na ukweli kuwa miji inakua lakini kuwapo na  vijiji na mitaa katika baadhi ya miji kama ya Dodoma MC, Ilemela MC, Tanga CC, Kasulu TC kunaleta changamoto, hivyo ipo haja ya kuangalia namna bora ya kubadili mifumo iliyopo.
Cartwright alisema suala si kufanya utafiti tu bali kuona nini kinatakiwa kufanywa kurekebisha makosa yaliyopo na kuwa na miji yenye utaratibu inayowezesha watu wake kuishi maisha bora.
Naye Dkt. Lolah Basolile ambaye ndiye Mwenyekiti wa mkutano huo uliofanyika ESRF - Dar es Salaam alisema kwamba kuna safari ndefu sana ya kuwa na mwongozo wa majiji nchini na kuwezesha miji kubadilika kwa namna inavyofaa katika kasi iliyopo.
Alisema kwa kutengeneza mwongozo itaweza kujulikana kitaifa ni namna gani maeneo yetu yatabadilika kuwa miji na majiji yenye hadhi katika utaratibu wa kuwezesha miundombinu na huduma stahiki.
Alisema shughuli za kuweka taratibu za miji haziwezi kufanywa na serikali pekee au watu binafsi pekee bali zinatakiwa kufanywa kwa ushirikiano.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: