Nchi waandaji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027) ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda zimesaini hati ya makubaliano ya pamoja inayojulikana kama CAF Joint Resolution – TotalEnergies AFCON PAMOJA 2027, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika maandalizi ya mashindano hayo makubwa barani Afrika.
Utiaji saini wa makubaliano hayo umefanyika Mei 11, 2026 na kushuhudiwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Patrice Motsepe, ambaye amepongeza hatua hiyo kuwa muhimu katika kuhakikisha maandalizi yanaenda kwa ufanisi na mshikamano miongoni mwa nchi hizo tatu.
Tanzania iliwakilishwa katika hafla hiyo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda pamoja na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiongozwa na Rais wa TFF, Wallace Karia.
Makubaliano hayo yanatarajiwa kusaidia uratibu wa maandalizi ya miundombinu, usafiri, usalama na masuala mengine muhimu kuelekea AFCON 2027, huku yakionesha dhamira ya Tanzania, Kenya na Uganda kushirikiana kwa karibu kuhakikisha mashindano hayo yanafanikiwa kwa viwango vya kimataifa.




Toa Maoni Yako:
0 comments: