Zanzibar, Aprili 2, 2026 — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko mbalimbali serikalini kwa kufanya uteuzi, uhamisho, utenguzi na upangaji wa vituo kwa viongozi kadhaa wa ngazi za juu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bakari S. Machumu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, mabadiliko hayo yamelenga kuimarisha utendaji kazi wa Serikali na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Katika uteuzi huo, Profesa Palamagamba John Aidan Kabudi ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), akitokea Ofisi ya Rais – Ikulu alikokuwa akihudumu katika kazi maalum.

Aidha, Mbunge Reuben Nhamanilo Kwagilwa amehamishwa na kuteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), huku Festo John Dugange akiteuliwa kuwa Naibu Waziri TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya elimu.

Katika hatua nyingine, Balozi Ali Jabir Mwadini ameteuliwa kuwa Katibu wa Rais, wakati Dkt. Eveline Wilbard Munisi na Bi. Angela Kizigha wameteuliwa kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vilevile, Balozi Said Othman Yakub amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, huku uteuzi wa Dkt. James Andilile Mwainyekule kama Mkurugenzi Mkuu wa EWURA ukitenguliwa ili kupangiwa majukumu mengine.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uapisho wa viongozi walioteuliwa utafanyika katika tarehe itakayopangwa baadaye.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: