Nairobi, Kenya — Rais wa Kenya, William Ruto, amekutana na wasanii wa muziki wa Gengetone na Urbantone na kusikiliza changamoto zao, hususan kupoteza haki za kazi zao kutokana na mikataba tata na taasisi za nje.

Katika mazungumzo hayo, wasanii hao walieleza kuwa wamepoteza zaidi ya nyimbo 700, ikiwemo wimbo maarufu Sipangwingwi wa msanii Exray, uliokuwa na ushawishi mkubwa mwaka 2022.

Rais Ruto alieleza kusikitishwa na hali hiyo, akibainisha kuwa ni jambo lisilokubalika kwa wasanii wenye vipaji vikubwa kuendelea kukumbwa na unyonyaji licha ya mchango wao katika kukuza utamaduni wa taifa.
Alisema tayari amechukua hatua kwa kuwezesha msaada wa kisheria kwa wasanii hao ili kuhakikisha wanapata uwakilishi sahihi mahakamani, sambamba na kuweka mikakati ya kulinda maslahi yao na kuhakikisha wanapata malipo stahiki kwa kazi zao.

Aidha, Rais huyo ameielekeza Bunge la Taifa kupitia Kiongozi wa Wengi kuharakisha kupitishwa kwa Muswada wa Uchumi wa Ubunifu wa mwaka 2026 pamoja na kufanya maboresho ya sheria za hakimiliki, hatua alizosema ni muhimu katika kulinda sekta ya ubunifu nchini humo.
Katika hatua nyingine, Serikali ya Kenya imeanzisha mfumo wa kidijitali kupitia jukwaa la e-Citizen utakaosaidia ukusanyaji na usambazaji wa mirabaha kwa wasanii kwa uwazi na ufanisi zaidi.

Hatua hizo zinatarajiwa kuimarisha ulinzi wa haki miliki, kuongeza mapato ya wasanii na kuweka mazingira bora kwa ukuaji wa sekta ya ubunifu nchini Kenya.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: