
Zurich — Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, limetangaza rasmi makundi ya michuano ya FIFA World Cup 2026, huku timu kubwa zikitarajiwa kukutana mapema katika hatua ya makundi.
Katika upangaji huo, Kundi C linaonekana kuwa moja ya makundi magumu likizikutanisha Brazil, Morocco, Haiti na Scotland, huku Kundi F likiwa na ushindani mkali kati ya Uholanzi, Japan, Sweden na Tunisia.
Kwa upande mwingine, mabingwa wa zamani Argentina wamepangwa Kundi J pamoja na Algeria, Austria na Jordan, wakati Ufaransa wakiwa Kundi I wakisindikizwa na Senegal, Iraq na Norway.
Kundi K nalo limevuta hisia baada ya kuzikutanisha Ureno, DR Congo, Uzbekistan na Colombia, wakati England wao wako Kundi L pamoja na Croatia, Ghana na Panama.
Barani Afrika, timu kadhaa zimepata nafasi ya kushiriki, zikiwemo Morocco, Tunisia, Senegal, Algeria, Ghana, Ivory Coast, pamoja na DR Congo, hatua inayoonesha kuongezeka kwa uwakilishi wa bara hilo katika michuano hiyo mikubwa duniani.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya timu zinazoshiriki, huku yakihusisha mataifa mbalimbali yenye historia kubwa ya soka.
Kombe la Dunia 2026 linatarajiwa kuvutia mashabiki mamilioni duniani kote, huku timu zikianza maandalizi ya mwisho kuelekea michuano hiyo itakayokuwa ya kipekee katika historia ya soka duniani.


Toa Maoni Yako:
0 comments: