Dar es Salaam — Tanzania inatarajiwa kushiriki mbio maalum za kuelimisha jamii kuhusu usonji kupitia Run 4 Autism Tanzania Half Marathon Season V, zitakazofanyika Aprili 4, 2026 katika viwanja vya Oysterbay Primary School.
Tukio hilo linafanyika sambamba na maadhimisho ya mwezi wa uelimishaji wa usonji duniani, ambapo leo Aprili 2 huadhimishwa kama Siku ya Uelewa wa Usonji Duniani.
Mbio hizo zinalenga kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu usonji, huku kauli mbiu ikiwa “Usonji na Ubinadamu – Kila Maisha Yana Thamani.”
Waandaaji wamewahamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki tukio hilo muhimu la kijamii na kiafya.



Toa Maoni Yako:
0 comments: