NaDodoma, Machi 31, 2026 — Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngwaru Jumanne Maghembe, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wawekezaji kutoka kampuni ya Liaoning Fangda wanaotaka kuwekeza nchini Tanzania.

Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dodoma, ambapo ujumbe huo ulioongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Ao Xinhua, uliwasilisha nia yao ya kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, usafirishaji wa anga na madini.
Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Maghembe aliwashukuru wawekezaji hao kwa kukubali mwaliko wa Serikali ya Tanzania na kufika nchini kujionea fursa zilizopo, akiahidi kuwa Serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha uwekezaji huo unafanikiwa.

“Serikali iko tayari kushirikiana nanyi bega kwa bega ili kuhakikisha miradi yenu inatekelezwa kwa ufanisi na kwa manufaa ya pande zote,” alisema Dkt. Maghembe.

Ujumbe huo ambao umekuwa nchini tangu Machi 25, 2026, umetembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam, ambapo umekutana na viongozi na wataalamu tofauti kwa lengo la kuchunguza fursa za uwekezaji.
Kwa upande wao, wawekezaji hao waliishukuru Serikali kwa mapokezi na ushirikiano walioupata, wakiahidi kurejea nchini kwa ajili ya kuanza uwekezaji rasmi katika sekta walizozitaja.

Ujio wa ujumbe huo umetajwa kuwa ni matokeo chanya ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo, aliyoifanya nchini China mwezi Juni 2025, ambapo alikutana na viongozi wa kampuni hiyo na kuwahamasisha kuja kuwekeza Tanzania.

Hatua hiyo inatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja na kuongeza ajira kupitia uwekezaji wa kimataifa.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: