Nairobi, Kenya — Rais wa Kenya, William Ruto, ameipongeza International Monetary Fund (IMF) kwa kuendelea kushirikiana na nchi hiyo katika kuimarisha uthabiti wa uchumi na kusaidia uwekezaji katika sekta za kipaumbele.
Rais Ruto alitoa pongezi hizo alipokutana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa IMF, Abebe Selassie, katika Ikulu ya Nairobi, ambapo viongozi hao walijadili hali ya uchumi wa Kenya pamoja na hatua za kuimarisha nidhamu ya matumizi ya serikali.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Selassie alieleza kuridhishwa kwake na namna Kenya inavyosimamia uchumi wake, hususan katika kudhibiti matumizi ya serikali (fiscal consolidation) na kuimarisha mifumo ya kifedha.
Aidha, mazungumzo hayo yaligusia pia athari za mgogoro wa vita katika eneo la Ghuba (Gulf), ambapo viongozi hao walijadili madhara yake kwa uchumi wa Afrika na dunia kwa ujumla, pamoja na mbinu za kupunguza athari hizo kwa wananchi.

Rais Ruto alimshukuru Selassie kwa uongozi wake thabiti ndani ya IMF na mchango wake mkubwa kwa nchi za Afrika, akimtakia mafanikio mema katika majukumu yake yajayo baada ya kuondoka katika taasisi hiyo.






Toa Maoni Yako:
0 comments: