Na Mwandishi Wetu -Narok, Kenya.

Rais wa Kenya, William Ruto, amempongeza mwanasiasa David Keter maarufu kama Dollarline kwa kushinda katika kura za mchujo za chama cha United Democratic Alliance (UDA) katika Jimbo la Emurua Dikirr Constituency.

Kupitia ujumbe wake, Rais Ruto alimpa pongezi Keter kufuatia ushindi huo muhimu uliompa tiketi ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo ujao wa jimbo hilo.

Aidha, Rais Ruto alimpongeza pia mpinzani wake Bernard Ng'eno maarufu kama Buluu kwa kuendesha kampeni imara, akieleza kuwa ushindani huo umeimarisha misingi ya demokrasia ndani ya chama hicho kuanzia ngazi za chini.

“Tunapongeza ushindani wa haki na wa kidemokrasia uliofanyika, ambao unaimarisha chama chetu na kuonesha mshikamano wa wanachama,” ilieleza sehemu ya ujumbe wa Rais Ruto.

Rais huyo alisisitiza kuwa baada ya mchakato wa mchujo kukamilika, ni muhimu kwa wanachama wote wa UDA kuungana na kumuunga mkono mgombea aliyepitishwa ili kuhakikisha ushindi katika uchaguzi mdogo.

“Tunakwenda mbele kama timu moja imara, tukiwa tumeungana nyuma ya mgombea wetu na ajenda ya chama,” aliongeza.

Ushindi wa Keter unatarajiwa kuongeza ushindani mkali katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, huku chama cha UDA kikilenga kuimarisha nafasi yake kisiasa katika Kaunti ya Narok na maeneo ya jirani.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: