Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Denis Londo, amesema Tanzania iko tayari kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Austria katika kukuza sekta za viwanda na biashara kwa manufaa ya pande zote mbili.

Akizungumza Machi 23, 2026 jijini Dar es Salaam, Mhe. Londo alisema hayo wakati alipokutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria, Hannah Liko, ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Mhe. Londo alieleza kuwa ziara hiyo ni hatua muhimu katika kufungua milango ya fursa za kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili, akisisitiza kuwa Tanzania imejipanga kwa kuweka mazingira rafiki na salama kwa wawekezaji wa kimataifa.

Alitoa wito kwa wawekezaji kutoka Austria kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda, kilimo, biashara na madini ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.
Aidha, alibainisha kuwa kutokana na kasi ya mapinduzi ya viwanda duniani, kuna umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika kubadilishana teknolojia, ujuzi na utaalamu ili kuongeza tija na ushindani wa kiuchumi.

Kwa upande wake, Dkt. Liko alisema Austria imejipanga kuendelea kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania katika sekta za elimu, ajira na utalii, huku akiipongeza Serikali ya Tanzania kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya.
Aliongeza kuwa Austria itaendelea kutoa ufadhili wa masomo kwa Watanzania pamoja na kuendeleza ushirikiano na Arusha Technical College (ATC), ikiwa ni sehemu ya Mkakati wa Afrika wa Austria (2026–2029).

Hatua hiyo inaonesha dhamira ya nchi hizo mbili kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi, sambamba na kukuza maendeleo endelevu kupitia sekta za umma na binafsi.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: