Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Simon Simalenga, Machi 10, 2026 ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika wilayani humo kwa lengo la kujadili rasimu ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027.

Katika kikao hicho, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi pamoja na Halmashauri ya Mji wa Bariadi na taasisi mbalimbali za serikali zilizopo wilayani humo ziliwasilisha rasimu za mipango na bajeti zao kwa ajili ya kujadiliwa na wajumbe wa kikao hicho.

Wajumbe walipata fursa ya kutoa maoni, ushauri na mapendekezo mbalimbali kuhusu mawasilisho hayo ili kuboresha mipango iliyowasilishwa na kuhakikisha inatekelezeka kwa ufanisi na kuleta maendeleo kwa wananchi wa Wilaya ya Bariadi.Akiwasilisha taarifa ya bajeti, ilielezwa kuwa katika mwaka wa fedha 2026/2027, Halmashauri ya Mji wa Bariadi imekadiria kukusanya jumla ya shilingi 4,171,764,000 kutoka vyanzo vya mapato ya ndani, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.97 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.

Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali kutoka Halmashauri ya Wilaya na Mji wa Bariadi, viongozi wa taasisi za serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wakuu wa idara na vitengo vya serikali wilayani humo.

Viongozi hao walisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika utekelezaji wa mipango na bajeti ili kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Wilaya ya Bariadi.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: