Na Mwandishi Wetu

Dar es Salaam, Februari 27, 2026: Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeandaa futari maalum kwa wateja na washirika wake ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha mahusiano na kuonesha shukrani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mkusanyiko huo uliwakutanisha wateja, wadau pamoja na viongozi wa kampuni katika mazingira ya umoja na mazungumzo ya karibu, yakilenga kuimarisha ushirikiano unaochangia mafanikio ya shughuli za kampuni nchini. Futari hiyo ilielezwa kuwa ishara ya kuthamini wateja ambao mchango wao wa muda mrefu unaendelea kuwa nguzo muhimu ya ukuaji wa kampuni.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Fatma M. Abdallah, alisema mkusanyiko huo ni njia ya kutambua nafasi ya wadau katika safari ya kampuni.

“Ramadhani ni kipindi cha kuonesha shukrani na kuthibitisha upya dhamira yetu ya kutoa huduma kwa uadilifu, ushirikiano na uwajibikaji kwa jamii,” alisema.
Kwa upande wake, Sheikh Mkowe Abdallah alisisitiza umuhimu wa mshikamano katika kipindi cha Ramadhani, akibainisha kuwa futari za pamoja huimarisha uhusiano wa kijamii na kuhimiza maadili ya huruma, heshima na uadilifu.

Mbali na tukio hilo, kampuni hiyo imeendelea kupanua uwekezaji wake katika nishati mbadala nchini, ikiwemo mradi wa gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) jijini Dar es Salaam unaolenga kuongeza upatikanaji wa mafuta safi na nafuu kwa magari ya abiria na mizigo. Mradi huo pia umechangia ajira kwa mamia ya Watanzania pamoja na kushirikisha wakandarasi wa ndani na biashara ndogo na za kati.

Akihitimisha, Mkuu wa Idara ya Sheria na Mahusiano wa kampuni hiyo, Emmanuel G. Bakilana, alisema mikusanyiko kama hiyo ni sehemu ya kujenga biashara yenye maadili na ushirikiano wa kudumu.

Alisema futari hiyo imeonesha wazi dhamira ya kampuni ya kuendelea kuimarisha mahusiano na wadau wake huku ikiunga mkono maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini kupitia uwekezaji katika miundombinu ya nishati.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: