Na Mwandishi Wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, ametangaza kuwa mkoa huo utakuwa mwenyeji wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) kitaifa mwaka 2026.
Mtaka ametoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa. Amesema mkoa umepokea nafasi hiyo kwa heshima kubwa na kuwaagiza wananchi kuitumia fursa hiyo kiuchumi kwa kufanya biashara mbalimbali, kwani zaidi ya wageni 5,000 wanatarajiwa kuhudhuria maadhimisho hayo.
“Mkoa tumepokea kwa heshima kubwa kuwa mwenyeji wa Mei Mosi kitaifa. Nawaomba wananchi wa Njombe kulichukulia jambo hili kama fursa ya kufanya biashara, kwa sababu ni matukio yanayovutia na kukusanya watu wengi,” amesema Mtaka.
Amewaagiza wenyeviti wa mitaa kuhakikisha wanazingatia usafi katika maeneo yao ili mkoa uwe katika hali nzuri ya kupokea wageni.
Kwa upande wake, Rais wa Nyamhokya,, Tumaini Nyamhokya, amesema wamepokea barua rasmi kutoka Serikalini kuthibitisha kuwa maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa mwaka 2026 yatafanyika Njombe. Nyamhokya amewahimiza wakazi kujiandaa kwa kuboresha huduma mbalimbali, ikiwemo huduma za chakula, ili kunufaika na fursa zitakazotokana na uwepo wa wageni wengi.



Toa Maoni Yako:
0 comments: