Na Mwandishi Wetu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum katika shule ya Msingi Mazinyungu, Wilayani Kilosa ikiwa ni sehemu ya tukio la kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Januari 27, 2026.

Zawadi hizo zilizokabidhiwa na Mkuu wa Wilaya Kilosa Shaka Hamdu Shaka ni pamoja na Magodoro, Mashuka,Vyandarua, Sabuni za kufuli na kuogea, Mafuta maalum kwa wenye ulemavu wa ngozi pamoja na Chakula.

Tukio hilo adhimu ni sehemu ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alizaliwa tarehe 27 Januari, 1960 katika Kijiji cha Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. 

Watoto hao wenye uhitaji maalum pia walikata keki ikiwa ni ishara ya kuungana na Mhe Rais Samia katika siku yake hii kwenye safari ya maisha yake.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: