Na Mwandishi Wetu, RUVUMA.

CHAMA cha National League For Democracy (NLD) kimempitisha Mhagama Hamisi Yusufu kuwania Ubunge Jimbo la Peramiho Mkoani Ruvuma ambayo ataipeperusha Bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa mdogo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Jenista Mhagama.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa,Katibu wa NLD Doyo Hassan Doyo ambapo aliwaambia kwamba siku hiyo ni muhimu kwa wananchi wa Jimbo la Peramiho kufanya maamuzi ya kiongozi wanayemtaka .

Alisema kwamba kiongozi ambaye anaweza kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo hilo ni mgombea wao kutokana na uongozi uliopita kwa miaka mingi umeshindwa kuwapa maendeleo na mabadiliko katika Jimbo hilo.

Katibu huyo aliwataka wananchi hao kutokufanya makosa katika uchaguzi huo wa marudio kutokana na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kufariki dunia hivyo aliwataka kumchagua mgombea anayetokana na NLD ili aweze kuwapa maendeleo makubwa.

Katika uchaguzi huo Mhagama Hamis Yusuf wa NLD atachuana na wagombea wengine akiwemo Yusuf Rashid Rai wa Chama cha AAFP,Abdallah Boniface Ngonyani wa Chama cha Makini,Hanifa Sembe Mohamed wa Chama cha UMD,Beatrice Omari Muya wa UPDP,Mapunda wa Chama cha DP,Dastan Frolian Pili wa CCK,Morice Thomas Nkongo wa TLP na Mtemi Pachoto wa UDP.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: