Na Mwandishi Wetu, Kibaha.

Diwani wa Kata ya Picha ya Ndege Mhe. Grace Jungulu amefanya ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakikisha maendeleo ndani ya Kata hiyo yanaenda kwa kasi 

Mhe. Jungulu ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa madarasa mapya yanayoendelea kujengwa katika Shule ya Sekondari Picha Ya ndege.

Katika ziara hiyo, Mhe Jungulu ametembelea pia Mradi wa Ujenzi wa fremu za biashara unaojengwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha pamoja na mradi wa Ufyatuaji wa tofali, Gereji na Eneo la kuosha magari (car wash).

"Mradi huo mkubwa uliopo katika Mtaa wa Muharakani utaenda kuing'arisha Kata ya Picha ya Ndege na kuongeza mapato na ajira kwa vijana," amesema Mhe Jungulu.

Aidha, Mhe Jungulu ametembelea Maeneo mbalimbali ya Mtaa Wa Lulanzi na kukagua miundombinu mbalimbali.

Mhe. Jungulu ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za ujenzi wa Miundombinu mbalimbali ikiwemo mashule, hospital, barabara za ndani ambapo utekelezaji wake unaenda kuleta maendeleo ndani ya Kata ya Picha ya Ndege.

Diwani  Kata ya Picha ya Ndege
 Mhe. Grace Jungulu akikagua mradi wa Ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari Picha ya Ndege ili
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: