RUDISHIWA NAULI YAKO! Mteja wa Vodacom Tanzania Plc, Regina Mbalamwezi akirudishiwa nauli yake baada ya kukata tiketi ya basi kupitia M-Pesa kutoka Dar es Salaam Kwenda Morogoro wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Shangwe Popote Ukitumia M-Pesa’ katika kituo cha mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam.
SHANGWE POPOTE! Mkurugenzi wa Biashara kutoka Vodacom Tanzania, Brigita Shirima akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kampuni hiyo ya ‘Shangwe Popote Ukitumia M-Pesa!’ lenye lengo la kuhamasisha wateja wake kufanya miamala yao kutumia M-Pesa wakati wa msimu huu wa sikukuu. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni.
SHANGWE LA SIKUKUU! Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Biashara kutoka Vodacom Tanzania, Brigita Shirima (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa ‘Shangwe Popote Ukitumia M-Pesa’ uliofanyika kituo cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Uzinduzi wa kampeni kabambe ya 'Shangwe Popote Ukilipa Kwa M-Pesa' ambayo inahamasisha wateja wa Vodacom kufanya miamala kupitia M-Pesa'.
Toa Maoni Yako:
0 comments: