Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Mheshimiwa Jenista Mhagama akifugua kikao cha mazingativu (Retreat) cha Menejimenti na Watumishi wa ofisi hiyo na Taasisi zilizopo chini yake kilichofanyika jijini Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Mheshimiwa Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wakuu ya wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo, baada ya ufunguzi wa kikao cha mazingativu (Retreat) cha Menejimenti na Watumishi wa ofisi hiyo na Taasisi zilizopo chini yake kilichofanyika jijini Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Mheshimiwa Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wakuu ya wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo, baada ya ufunguzi wa kikao cha mazingativu (Retreat) cha Menejimenti na Watumishi wa ofisi hiyo na Taasisi zilizopo chini yake kilichofanyika jijini Arusha.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) wakifuatilia jambo katika kikao cha mazingativu (Retreat) cha Menejimenti na Watumishi wa ofisi hiyo na Taasisi zilizopo chini yake kilichofanyika jijini Arusha.

Na; Mwandishi Wetu – Arusha.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Mheshimiwa Jenista Mhagama, amewataka watumishi wa Ofisi hiyo kuzingatia vipaombele ambavyo ni muhimu kupewa msukumo katika utekelezaji wa shughuli kwa mwaka wa h 2024/25.

Ameyasema hayo mapema leo tarehe 31 Julai, 2024 Jijini Arusha alipokuwa akifungua kikao kazi cha Mazingativu (Retreat) kilichohusisha watendaji na watumishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) pamoja na Taasisi zake.

Akiongelea kipaumbele cha kwanza ambacho ni Kuratibu Ujenzi wa Majengo ya Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba, Waziri Mhagama alisema, Ofisi ya Waziri Mkuu katika mwaka wa fedha 2024/25 itaendelea na uratibu wa ujenzi wa majengo ya Ofisi za Wizara, Taasisi pamoja na miundombinu mbalimbali katika Mji wa Serikali wa Mtumba, pamoja na kutoa vibali vya ujenzi kwa Taasisi za Serikali zinazoendelea kuhamia Makao Makuu ya Chama na Serikali Dodoma, ikiwa na nia kuhakikisha kuwa Awamu ya Tatu ya ujenzi wa Mji wa Serikali inakamilika kwa wakati na watumishi wanahamia katika majengo hayo ndani ya mwaka wa fedha 2024/25 na kuelekeza kuwa Uratibu huo uimarishwe sambamba na kuweka ufuatiliaji wa karibu wa ujenzi pamoja na ununuzi wa samani za majengo yote.
Akiongelea suala la Kuimarisha Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Shughuli za Serikali, Waziri Mhagama Alibainisha kuwa, Kulingana na muundo mpya wa Ofisi ya Waziri Mkuu ipo Idara mpya iliyoundwa ambayo jukumu lake kubwa ni kusimamia masuala yote ya Tathmini na Ufuatiliaji wa Utendaji wa Serikali kwa ujumla kuanzia ngazi za Wizara na taasisi zake, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Aidha Waziri Mhagama Aliipongeza Idara hiyo kwa kazi kubwa inayoendelea kuifanya na kusema kuwa hadi saa imeandaa Mwongozo wa Ufuatiliaji na Tathmini nchini na imekamilisha Mwongozo wa Menejimenti ya Tathmini nchini na Mwongozo wa kufanya tathmini ya utayari wa masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini katika Taasisi za Serikali.

“Baada ya kazi hiyo nzuri sasa tunahitaji kuona matokeo ya utendaji unaotokana na kuimarishwa kwa ufuatiliaji na tathmini, Masuala mbalimbali ambayo ni muhimu kutiliwa mkazo ni ufuatiliaji wa maoni na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambayo hutoa mwelekeo wa utendaji wa Serikali.”

Alisisitiza Waziri Mhagama.Aliendelea kusema kuwa, Hatua hii itajenga imani zaidi kwa wadau kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kudhibiti matumizi mabaya ya mali za umma na kuelekeza kazi ya kukamilisha Mfumo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Shughuli za Serikali (Government Wide Integrated Monitoring and Evaluation System) ikamilike mapema kabla ya mwezi Disemba, 2024 na ili mfumo huo uanze kufanya kazi na kuwezesha upimaji wa utendaji wa Serikali kufanyika kwa urahisi, haraka na ufanisi mkubwa.

Akiongelea kuhusu Kuimarisha Uwezo wa Uchapishaji wa Nyaraka za Serikali, Waziri Mhagama alipongeza jithada za maboresho yanayoendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda kipya, ununuzi wa mashine mpya saba na matengenezo ya mashine zaidi ya 13.

“Nawapongeza wataalam waliobuni na kuandaa maandiko yaliyowezesha kupata mafanikio haya kwa muda mfupi, Naendelea kutoa wito kuwa shughuli za uchapaji wa nyaraka zote za Serikali ufanywe na Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali na ufuatiliaji ufanyike kwa Taasisi ambazo zinakiuka masharti ya Waraka uliotolewa kwa Watendaji wote.”

Alisisitiza Waziri Mhagama.Akizungumza kuhusiana na Vita dhidi ya biashara haramu na Matumizi ya Dawa ya kulevya, Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo kupongeza hatua mbalimbali za udhibiti wa dawa za kulevya nchini akitolea mfano wa mafanikio yaliyopatikana na kusema kuwa ni kiashiria kikubwa cha utendaji mzuri wa Mamlaka ya kuthibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini.

“Dhahiri kwamba nchi yetu imejipatia heshima ndani na nje ya nchi kwa kuwa na mifumo imara ya udhibiti wa dawa za kulevya na tumeweza kuwalinda watu wetu dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.” Alisema

Aidha, Waziri Mhagama alibainisha kuwa, ni azma ya Serikali ya Awamu ya Sita (6) chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kuwa biashara ya dawa ya kulevya inakomeshwa, kwani ina madhara makubwa sana kwa jamii ya Watanzania na inaathiri nguvu kazi ya Taifa na kutoa wito wa kuendeleza jitihada za kuendeleza mapambano, sambamba na kuweka msukumo wa utekelezaji wa Sera mpya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya mwaka 2024.

Akiongelea suala la Usimamizi na uratibu wa masuala ya Uchaguzi, Waziri Mhagama alisema, Mwaka huu wa 2024 na mwaka 2025 kutafanyika chaguzi mbalimbali, Mwaka 2024 kutafanyika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Mwaka 2025 utafanyika Uchaguzi Mkuu.

“Chaguzi hizi zinahitaji maandalizi ya kutosha na uratibu mzuri, hivyo nitoe wito kwa Taasisi inayohusika na maandalizi ya Uchaguzi pamoja na Idara ya Bunge na Siasa kufanya maandalizi na uratibu kwa ukamilifu ili kufanikisha chaguzi hizi.”

Akihitimisha hotuba yake alitumianfursa hiyo kutoa pole kwa wananchi waliopatwa na maafa ya Mafuriko mwishoni mwa mwaka 2023 hadi mwezi Aprili, 2024, na Mvua za El Nino, na kusema kuwa Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na maafa hayo.

“Nitumie fursa hii kupongeza jitihada zilizochukuliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika kukabiliana na maafa hayo, Tuendelee kufanya kazi kama Timu ili kupata matokeo makubwa zaidi katika kukabiliana na majanga huku jitihada kubwa zikielekezwa katika utoaji wa elimu kwa umma.”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: