Na Mwandishi Wetu

TUME ya Ushindani  (FCC) imewahakikishia  wawekezaji kutoka nje ya nchi  wanaokuja  nchini Tanzania kuwekeza  kwani kuna mazingira salama ya uwekezaji pamoja na kufanyabiashara.

Hayo yamesemwa  jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio alipokuwa akizungumza  na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Kudhibiti  bidhaa bandia duniani ambayo huadhimishwa kati ya Juni na Julai ya kila.

Amesema Serikali  ya Awamu ya Sita imekuwa ikihimiza wawekezaji kutoka nje kuja nchini ili kufanya uwekezaji pamoja na biashara sambamba na kudhibiti ubora.

Kuhusu ubora wa bidhaa ,Erio amewashauri wananchi kuacha mara moja matumizi ya bidhaa bandia na badala yake wanunue na kutumia bidhaa halisi ili kusaidia kuchochea uwekezaji, kukuza fursa za ajira na hatimaye kuchagiza ukuaji wa uchumi wao na taifa kwa ujumla.

“Tusikubali kununua bidhaa bandia na hii itasaidia hata wale wanaokuja kuwekeza watakapofanya tathimini ya bidhaa zilizopo wakute tunatumia bidhaa halisi na zilizobora."

Pia amesema kati ya asilimia 2.5 na 3.5 ya biashara zinayofanyika ulimwenguni zinahusisha bidhaa bandia huku akibainisha baadhi ya madhara ya bidhaa hizo kuwa ni kutopata thamani halisi ya fedha pamoja na madhara mbalimbali ya kiafya kwa watumiaji

Akizungumzia Wiki ya kudhibiti bidhaa bandia duniani amesema wiki hiyo  inaadhimishwa sehemu zote duniani kati ya Juni na Julai na sababu yake ni kwamba bidhaa bandia zina changamoto nyingi.

Ametaja baadhi ya athari za bidhaa bandia  kuzorotesha  biashara, uchumi na kukosena kwa ajira nchini."Bidhaa bandia zina matatizo hata katika maeneo ya kiuchumi kwanza zinaathiri ubunifu kwasababu katika kushindana unatakiwa kila kitu uje na kitu kipya kuwa na bidhaa katika uchumi kunadhorotesha biashara.

Katika maadhimisho ya mwaka huu kauli  mbiu inasema Kudumisha uhalisia kwa kulinda ubunifu kwa maendeleo ya kiuchumi nchini na inatarajiwa kuadhimishwa Julai 18 katika ukumbi wa mikutano ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Pia katika maadhimisho hayo  kutakuwa na  maonyesho mbalimbali ya wajasiriamali na wamiliki wa viwanda vidogovidogo pamoja na majadiliano ya jopo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio akiteta jambo na wadau wa tume hiyo,
Mkutano ukiendelea.

PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: