(Kushoto Kwenda Kulia) Mheshimiwa Bw. Rohit Vadhwana, Kaimu Kamishina Mkuu wa India, Sharad Malhotra - Makamu wa Rais Mkuu, Nipsea Group, Hardev Singh- Rais na Mkurugenzi (Idara ya Kiwanda), Nippon Paint India, Arun Mishra - Meneja Biashara, Nipsea Paint Kenya, Jamil Virjee, Mkurugenzi Mtendaji wa Coat It, Diwakar Mehrotra, Makamu wa Rais, Nippon Paint GroupAR
(Kushoto Kwenda Kulia) Sharad Malhotra - Makamu wa Rais Mkuu, Nipsea Group na Mheshimiwa Bw. Rohit Vadhwana, Kaimu Kamishina Mkuu wa India wakimkabidhi Irene - Mkuu wa Mahesabu Mogra Rescue Center na Simon – Mkuu wa Uendeshaji Morga Rescue Center mchango wa KSH 500,000.

Na Mwandishi Wetu.

Dar es Salaam, Tanzania, Julai 8, 2024 - Nippon Paint, kampuni ya nne inayozalisha rangi kwa ukubwa duniani kwa mapato, imepiga hatua kubwa katika soko la Afrika Mashariki baada ya kuzinduliwa Nairobi Ijumaa, Julai 5. Kampuni tanzu inayomilikiwa, "NIPSEA Paint," itatambulisha teknolojia ya hali ya juu ya Kijapani ili kuboresha huduma kwa wateja katika urekebishaji wa magari, utunzaji wa gari, upakaji rangi mbao na wa viwandani.

Ikifanya kazi kupitia mfumo wa usambazaji, Nippon Paint imeifanya Nairobi kuwa kitovu chake kikanda, kabla ya kuanzisha shughuli zake katika nchi husika za Afrika Mashariki. Afrika Mashariki inaendelea kuwa kitovu cha biashara kinachokua, kikiwa na maendeleo madhubuti ya kiuchumi, tabaka la kati linalokua, na kuongezeka fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali.

"Tuna shauku ya kuanzisha uwepo wetu kwa mara ya kwanza barani Afrika kupitia Nairobi na Afrika Mashariki. Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, tumefanikiwa kuingiza bidhaa zetu sokoni kupitia msambazaji wetu, na mwitikio umekuwa wa kipekee. Kwa uwepo wetu wa moja kwa moja, ikijumuisha ofisi na sehemu ya kuhifadhia bidhaa zetu, tunathibitisha kujizatiti kwetu na kupanua utoaji wa bidhaa zetu ili kukidhi wateja wa aina tofauti kwa kila bei." Alisema Bw. Sharad Malhotra, Mkurugenzi wa Nippon Paint India na NIPSEA Paint.

Kimkakati, Afrika Mashariki ni muhimu kwa mipango ya upanuzi ya kimataifa ya Nippon Paint, kwasababu eneo hili linatoa fursa mbalimbali za soko zinazowiana na dira ya muda mrefu ya shirika kwa ukuaji uvumbuzi na endelevu.

"Uamuzi wa Nippon Paint wa kuanzisha uwepo wa moja kwa moja utaimarisha juhudi na rasilimali zetu zilizopo. Bidhaa za Nippon Paint zimepokelewa vizuri, na tunatarajia kukidhi zaidi mahitaji ya wateja na kuongeza wigo wa bidhaa na kuimarisha uwezo wa huduma." Bw. Jamil Virjee, Mkurugenzi Mkuu wa Coat It, mshirika wa usambazaji wa Nippon Paint kwa uboreshaji wa magari nchini Kenya, alielezea shauku yake kuhusu kuwepo sokoni moja kwa moja kwa Nippon Paint.

Nippon Paint, kampuni kubwa ya bidhaa za rangi katika ukanda wa Asia Pacific, linaingia katika soko la Afrika Mashariki likiwa na safu thabiti ya bidhaa zilizotengenezwa kulingana na hali ya soko la ndani. Kupitia mbinu ya kimfumo, kampuni inalenga kuinua viwango vya sekta kwa kuanzisha teknolojia ya hali ya juu, orodha ya bidhaa tofauti, na jitihada za mafunzo kwa wateja na kukuza ujuzi.

Utambulisho huu wa Nippon Paint unaenda sambamba na Maonesho ya Biashara ya Kimataifa - Saba Saba, jijini Dar es Salaam. Maonyesho haya, maarufu kote Afrika Mashariki kwa kukuza biashara ya kikanda na kubadilishana kitamaduni, yanasisitiza kukua kwa umuhimu wa Tanzania kama kitovu kikuu cha soko la biashara. Ahadi ya Nippon Paint kwa kanda ya Afrika Mashariki inaonyesha dhamira yake ya kushirikiana na wadau wa ndani na kukuza ushirikiano wa muda mrefu katika jumuiya ya biashara ya Afrika Mashariki. 

Shirika hilo linalenga kutambulisha bidhaa za ubora wa hali ya juu na za kiubunifu ambazo zitainua viwango vya sekta katika ukanda wote na kuwapa watumiaji chaguo bora zaidi, na kupelekea ukuaji na ustawi zaidi katika Afrika Mashariki.
 (Kushoto Kwenda Kulia) Arun Mishra – Meneja Biashara, Nipsea Paint Kenya, Angela Wambui – Kutoka Tasnia ya Vyombo vya Habari, Diwakar Mehrotra – Makamu wa Rais, Nippon Paint GroupAR.
(Kushoto Kwenda Kulia) Irene – Mkuu wa Mahesabu Mogra Rescue Center, Sharad Malhotra – Makamu wa Rais Mkuu, Nipsea Group, Simon – Mkuu wa Uendeshaji Morga Rescue Center.
(Kushoto Kwenda Kulia) Mheshimiwa Bw. Rohit Vadhwana, Kaimu Kamishina Mkuu wa India akitambuliwa na Sharad Malhotra - Makamu wa Rais Mkuu, Nipsea Group.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: