Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, Dkt. Said Mohamed

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE(CSEE) 2023 NA MTIHANI WA MAARIFA (QT) YAMETANGAZWA RASMI LEO ALHAMISI JANUARI 25,2024

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2023

MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2023

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv


BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani ya kidato cha nne uliofanyika Novemba 14 2023 Tanzania Bara na Visiwani ambayo yameonesha ufaulu umeongezeka kwa asilimia0.87 ukilinganisha na mwaka 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 25, 2024, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Said Mohamed amesema jumla ya watahiniwa 572,359 walisajiliwa kufanya mtihani wasichana 310,248 sawa na asilimia 54.21 na wavulana 262,111 sawa na asiilimia 45.79 ambapo kati ya watahiniwa hao, wa shule ni 543,332 na wa kujitegemea ni 29,027.

Amesema kati ya watahiniwa wa shule 543,332, watahiniwa 529,596 sawa na asilimia 97.47 ya waliofanya mtihani wavulana walikuwa 244,703 sawa na asilimia 97.80 na wasichana 284,893 sawa na asilimia 97.19 huku watahiniwa 13,736 sawa na asilimia 2.53 hawakufanya mtihani

Akizungumza kuhusu watahiniwa wa kujitegemea Dkt. Mohamed amesemaa, waliosajiliwa walikuwa ni 29,027 ambapo watahiniwa 25,626 sawa na asilimia 88.28 ndio walifanya mtihani huku watahiniwa 3401 sawa na asilimia 11.72 hawakufanya mtihani.

"Jumla ya watahiniwa 484,823 sawa na asilimia 87.65 ya waliofanya mtihani huu wamefaulu ambapo wasichana ni 257,892 sawa na asilimia 86.17 wakati wavulana ni 226,931 sawa na asilimia 89.40 ikiwa ni ongezeko la ufaulu kwa asilimia 0.87 ukilinganisha na mwala 2022 ambapo waliofaulu walikuwa 476,450 sawa na asilimia 86.78' amesema Dkt. Mohamed.

Amesema ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa Madaraja ya I - III ni 197,426 sawa na asilimia 37.42 wakati Mwaka 2022 watahiniwa waliopata ufaulu wa madaraja I – III walikuwa 192,348 sawa na asilimia 36.95. Hivyo, ubora wa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.46 ikilinganishwa na mwaka 2022.

"Ubora wa ufaulu ma madaraja ya I-III ni mzuri zaidi kwa wavulana ikilinganishwa na wasichana ambapo wavulana ni 108,368(44.47%) na wasichana ni 89,058(31.37%).

Aidha Dkt. Mohamed amesema kwa mwaka 2023 Masomo ya sayansi yamefanya vizuri huku somo la Hisabati likiendelea kutokufanya vizuri licha ya kuwa ufaulu umepanda.

" Na kwenye masomo ya sayansi somo ambalo limefanya vizuri ni chemisrty na Bialogy kwa kuwa Biology inafanywa na wanafunzi wote.

Katika ufaulu huu Asilimia 87 umetokana na shule za serikali huku asilimia 13 ukitokana na shule za Private.

Aidha, Baraza la Mtihani limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 376 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kumaliza mitihani yao ya kidato cha nne kwa mwaka 2023 kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.

Watahiniwa husika watapewa nafasi ya kufanya mitihani kwa masomo ambayo hawakufanya kwa sababu ya ugonjwa kwa mwaka 2024 kwa mujubu wa kifungu cha 32 (1) cha kanuni za mitihani

Pia Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 102 ambao wamebainika kufanya udanganyifu katika mitihani.

Aidha Wanafunzi 5 wamefutiwa kutokana na kuandika lugha ya matusi kwenye Mitihani

Na hawa wanafunzi 102 wamefanya uzembe wenyewe kwa kuingia na Karatasi Wengine simj na lakini wapo ambao wamesaidiwa na wamalimu kufanya Mtihani hivyo taratibu nyingine zinaendelea.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments:

Back To Top