Benki ya CRDB imetangazaushirikiano na kampuni ya kimataifa ya malipo ya American Express, ambao unawezesha Benki hiyo kupokea matumizi ya kadi za American Express katika mtandao wake na hivyokupanua wigo wa huduma za malipo kwa wateja wenye kadi hizo pindi watembeleapo nchini.
Ushirikiano huo ambao umeenda sambamba na uzinduzi wa matumizi ya kadi za American Express katika mtandao wa Benki ya CRDB ulitangzwa katika hafla maalum iliyofanyikakatika hoteli ya Gran Melia ambapo mgeni rasmi alikuwaMkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela ambayealipongeza hatua hiyo na kusema itasaidia kuvutia wageniwengi zaidi nchini.
Uzinduzi wa matumizi ya kadi hiyo unawezesha watejawenye kadi za American Express kutumia Kadi zao kufanyamalipo kwa urahisi katika sehemu mbalimbali za hudumanchini zenye vifaaa vya malipo vya Benki ya CRDB pamoja na malipo ya mtandaoni. Wateja pia wamewezeshwa kutoapesa taslimu kwenye ATM zinazofanya kazi kwenye mtandaowa Benki ya CRDB.
Tangu 2017, American Express imeongeza mara tatu zaidi ya maeneo ambayo yanaweza kukubali Kadi zake, ambapo sasahivi kadi hizo zinatumika katika maeneo milioni 80 dunianikote. Kukubalika kwa matumizi ya kadi hizi hapa nchinikutasaidia biashara zenye mfumo wa malipo wa Benki ya CRDB kuongeza wateja zaidi kutoka katika wigo mpana wa wateja wanaotumia kadi hizo sio tu kutoka Afrika bali dunianikote. Hii inajumuisha wageni na wateja wanaosafiri kwa ajili ya biashara, utalii, au kutembelea marafiki na familia.
Akizunguzuma katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha alisema uzinduzi wa matumizi wa kadi hizo utapelekea mazingira rafiki ya kufanya miamala kwa rahisi na usalama kwa wageni wanaotembelea nchini na katika mtindo waliouzoea, jambo ambalo linawajengea imani na kuwafanya wawe na hamu ya kurejea nchini na hivyo kuchochea utalii zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema Benki hiyo inafurahi kuwa mshirika wa American Express nchini Tanzania na kuwaruhusu wageni wa Kimataifa wenye kadi za American Express kutumia Kadi zao nchini. Nsekela alisema ushirikiano huu unawapa watalii na wafanyabiashara wakigeni wanaokuja Tanzania chaguo zaidi za malipo.
“Hivi karibuni tumeshuhudia kuimarika kwa sekta ya utalii kwa kiasi kikubwa jambo ambalo limepelekea idadi ya watalii kuongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuitangaza nchi na vivutio vyake. Makubaliano yetu na American Express yatasaidia kuwapa wageni uzoefu bora wa malipo pindi wawapo nchini, lakini pia yatafungua fursa mpya za biashara na kukuza wafanyabiashara wetu, ” alisema Nsekela.
Kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania ya Oktoba 2023 idadi ya watalii nchini imeongezeka kwa asilimia 63.5 mwezi Septemba mwaka huu kufikia 1,332,476 kulinganisha na kipindi kama hicho mwaka 2022. Mapato ya kutokana sekta ya utalii yameongezeka maradufu kufikia Dola za Marekani milioni 2,243.8 kutoka Dola za Marekani milioni 1,106 iliyorekodiwa mwaka 2022. Kadi ya American Express inatazamiwa kuvutia watalii wengi kuja nchini na kuchochea ukuaji wa mapato zaidi.
Briana Wilsey, Makamu wa Rais na Meneja Mkuu wa Masoko ya Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika American Express, alisema: "Tunafurahia leo hii kupanua zaidi idadi ya maeneo ambayo kadi zetu za American Express zitakuwa zikiweza kufanya duniani kote. Ushirikiano huu na Benki ya CRDB unawapa chaguo kubwa la malipo kwa wateja wenye kadi zetu zaidi ya milioni 135 wanaotembelea Tanzania kwa ajili ya utalii na biashara.”
Hafla hiyo ya uzinduzi wa matumizi ya kadi za American Express ilihudhuriwa na taasisi na wafanyabiashara wanaopokea malipo kupitia mfumo wa malipo wa Benki ya CRDB ikiwamo TANAPA, Makampuni ya Utalii, pamoja na Umoja wa Waongoza Watalii nchini (TTGA).
Wafanyabiashara ambao wanahitaji kupokea malipo ya kadi za American Express wanatakiwa kupiga namba ya bure 0800008000 au barua pepe info@crdbbank.co.tz au tembeleatovuti rasmi ya benki https://crdbbank.co.tz/en/product/business/accounts/28
Briana Wilsey, Makamu wa Rais na Meneja Mkuu wa Masoko ya Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika American Express (katikati) akifanya malipo katika kifaa cha manunuzi (PoS) kuashiria uzinduzi wa matumizi ya kadi za American Express katika mtandao wa Benki ya CRDBff. Wakishuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Prof Neema Mori, na Afisa Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Boma Raballa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: